Manchester United imethibitisha kuwa Juan Mata ataondoka katika klabu hiyo mkataba wake utakapokamilika msimu huu wa joto. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na Red Devils Januari 2014 na kucheza michezo 285, akifunga mabao 51 na kushinda mataji manne.

Mata anaungana na Paul Pogba Jesse Lingard katika orodha ya wachezaji wa Man United wanaondoka Old Trafford wakati wa dirisha la usajili majira ya joto

Mata alichapisha ujumbe wa video kutoka uwanja wa Old Trafford kufuatia kauli ya United, ambapo aliwashukuru mashabiki kwa sapoti yao ‘hasa katika nyakati ngumu’.

“Niko peke yangu. Kwa kweli hii najihisi kama ndoto,’ Mata alisema. ‘Nilitaka kusema asanteni sana kwenu nyote kwa msaada wenu kwa miaka mingi, hasa katika nyakati ngumu tulizoishi pamoja”.

Aidha, Wachezaji wengine wakiwemo Nemanja Matic na Edinson Cavani wanatarajiwa kuondoka Man. Utd wakati huu ambao Kocha mpya, Erik ten Hag ameadhimia kuijenga upya timu


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa