Sadio Mane alifunga hat-trick dhidi ya Benin na kuweka rekodi mpya akiwa na timu ya taifa katika ushindi wa 3-1 kwenye michuano ya kuwania kucheza AFCON 2023.

Mane amefikia hatua hiyo ya mabao 32 akiwa amecheza mechi 90 na timu ya taifa ambapo katika magoli matatu aliyofunga mawili alifunga kwa mikwaju ya penati.

Mafanikio ya kuvunja rekodi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 yanakuja huku kukiwa na uvumi mkubwa juu ya hatma yake baada ya msimu mwingine bora kwa kikosi cha Jurgen Klopp.

Siku ya Ijumaa, mshambuliaji huyo alifunguka kwamba atafanya kile ambacho watu wa Senegal wanataka afanye, huku kukiwa na ripoti kwamba anaweza kuwa njiani kuelekea Bayern Munich.

Orodha ya wafungaji bora wa muda wote timu ya taifa ya Senegal

1. Sadio Mane – 32
2. Henri Camara – 29
3. El Hadji Diouf – 24
4. Mamadou Diang – 20
5. Jules Bocande – 20
6. Moussa Bow – 18
7. Papiss Cisse – 17
8. Mamadou Diallo – 15
9. Mousa Konate – 12
10. Papa Bouba Diop – 11


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa