Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane ameleza kwamba alikuwa tayari na mkataba na Klabu ya Manchester United kabla kugeukia Liverpool wakati wa usajili wa mwaka 2016.

Mane alionyesha kiwango thabiti wakati akiitumikia Southampton kwenye Premier League hali iliyopelekea Manchester United kuhitaji huduma yake na Red Devils walidhani wapo peke yao kwenye mbio za kuinasa saini ya Mane lakini Klopp alimshawishi Msenegali kuwa Liverpool ndiyo mahali sahihi kwake.

“Nilikuwa karibu kujiunga na United nilikuwa na mkataba kule.” Alisema Mane.

“Nilikuwa nimekubaliana nao tayari, lakini badala yake nilifikiria, Hapana nataka kwenda Liverpool , nilishawishika na mradi wa Klopp. Bado nakumbuka nilivyopata simu ya Klopp kwa mara ya kwanza.

“Klopp alieleza jinsi alivyoshindwa kunisajili kipindi yupo na Dortmund na aliomba radhi kwa hilo nilimwambia ni sawa huwa inatokea.” Klopp alisema “Tuna mradi mkubwa hapa Liver na tunahitaji wewe pia uwe sehemu ya mradi wetu.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa