Kocha wa zamani wa Birmingham Marc Skinner ameteuliwa kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Manchester United kwa upande wa wanawake.
Skinner alitangaza kujiuzulu wadhfa wake huko Orlando Pride wiki iliyopita, na kumaliza uvumi kuwa alikuwa ni mbadala wa Casey Stoney.
Alhamisi United wamethibitisha uteuzi wake. Marc Skinner ambaye ana miaka 38 amesaini mkataba wa miaka miwili na United.
Kocha huyu alianza kazi yake kama kocha miaka nane iliyopita huko Birmingham, akipitia ngazi kadhaa na kufika Orlando Pride mwaka 2019.
Marc amesema kuwa anafurahi kuwa United na ni mpango wake kuhakikisha anashirikiana na uongozi kupata mafanikio makubwa klabuni hapo.
Makamu Mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward amesema kuwa wanamtambua Skinner kama mmoja wa makocha wenye uzoefu, ni furaha yao kumuona anarejea EPL baada ya kutumia mda fulani kwenye soka la Marekani.
SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!
Angelina
Kila kheri