Klabu ya Simba SC leo itashuka katika Uwanja wa Jenerali Senyi Kountche kuikabili US Gendarmarie Nationale ya Niger katika mchezo wa kwanza ugenini wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.

 

simba sc, Matchday : Simba SC vs US Gendarmarie., Meridianbet

Mchezo huo ni wa pili katika hatua ya makundi lakini ni wa kwanza ugenini baada ya Simba SC kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 jijini Dar es Salaam dhidi ya ASEC Mimosas.

Kikosi cha Simba kiliwasili jana katika mji wa Niamey ambapo mchezo utapigwa na wachezaji wote waliosafiri wako tayari kwa mchezo na kikosi kilifanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Jenerali Senyi Kountche.

Kocha wa Simba SC, Pablo Franco pamoja na kukiri mchezo utakuwa mgumu lakini ameweka wazi wanahitaji kushinda na kupata alama zote tatu na si kupoteza.

“Tutaingia katika mchezo wa leo kwa lengo la kutafuta pointi tatu muhimu ugenini, tusipofanikiwa tutahakikisha tunatafuta sare lakini si kupoteza.

 

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu, Gendarmerie wametoka kupoteza mechi ya kwanza na watataka kutumia vema uwanja wa nyumbani lakini tumejipanga kuwakabili,” amesema Pablo

Mchezo huo utapigwa majira ya saa moja usiku kwa saa za Tanzania na saa 11 jioni kwa saa za Niger.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa