Imebarikiwa ardhi ya Kongo anakotoka Mayele kwa rasilimali, achana kwanza na vivutio vyake, chini ya ardhi yake imefichwa dhahabu, almasi, copper, cobalt, tin na yale madini ya coltan.

Basi na miguu ya Mayele imebarikiwa kama ardhi ya nyumbani kwake. Ndani ya miguu yake miwili kuna maajabu, miujiza na uponaji.

Miguu wake wa kulia unatibu ‘presha’! Kivipi uugue presha wakati una uhakika atafunga bao la kusisimua sekunde yoyote ile mchezoni?

mayele
mayele

Ule wa kushoto unafukuza bahati mbaya, roho mbaya na makasiriko. Atakufunga kikatili halafu atakimbia kushangilia kwa kukuburudisha. Makasiriki yatatoka wapi??

Moyo mgumu wa kupambana na wazungu kama Patrice Lumumba, yule baba wa taifa la Congo alioitoa mikononi mwa wabelgiji. Jela, kuuawa kwa familia yake na mengine mengi bado alisonga mbele kuitoa Congo utumwani!

Ndivyo lilivyo soka la Mayele. Muweke gerezani na beki wako bora kuliko wote, mpige buti dakika zote kisha mtukane kila unapokumbana nae uwanjani, atasonga mbele kuipambania jezi ya timu yake.

Kama utemi wa wale waasi wa M23. Wale askari wa Betrand Bisimwa, Sultan Makenga na Jean Marie Runiga walioiteka Goma na kukataa mazungumzo na serikali,

Hivo ndivyo ilivyo roho ya Mayele mbele ya safu ya ulinzi ya wapinzani wake. Utemi! Ukatili! Utemi! Hakuna makubaliano ya amani kati yao. Nipe vita nikulipe hasara. Nipe ugomvi nikulipe maumivu.

Kama hatari ya volcano imwagiwayo katika milima ya Nyiragongo, kama ule moto ushukao na chemichemi za Lava zinazotisha kutoka katikati ya vilima vyake, basi ndivyo lilivyo soka la Mayele.

Ni hatari kwa wapinzani kila alitazamapo lango. Ni chemichemi ya lava kila aonapo nyavu. Ni moto kila amtazamapo golkipa.

Kama utunzi na ala zilizopangika katika mashairi ya Rumba ya Papa Wemba, kama wale wapiga gitaa wa ‘Zaiko Langalanga’ na kama wale wacheza kinanda wa ‘Yoka lokole’,

Basi ndivyo ilivyo burudani kumtazama Fiston Kalala Mayele. Anakufunga halafu anakuburudisha. Unavutiwa kumtazama machoni, unafurahia moyoni halafu unasisimka rohoni kwa soka lake.

Ndiyo maana nasema, nipe ramani ya Congo nikusimulie Fiston Mayele. Inavutia kumsimulia.

Imeandikwa na Deo Mwanasoka.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa