Mchezaji wa klabu ya Manchester City Benjamin Mendy amekana makosa nane yanayo mkabili ya unyanyasaji wa kijinsia.

Mendy Akana Mashitaka ya Ubakaji Yanayomkabili

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifika katika kikao cha kusikilizwa katika Mahakama ya Chester siku ya Jumatatu kuwasilisha maombi yake kwa mara ya kwanza.

Mendy anakanusha makosa saba ya ubakaji, shtaka moja la unyanyasaji wa kijinsia na moja la kujaribu kubaka.

Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 27 alishtakiwa kufuatia madai yaliyotolewa na wanawake sita, huku makosa hayo yakidaiwa kufanyika kati ya Oktoba 2018 na Agosti 2021.Beki Mendy atakabiliwa na kesi Julai 25.

Beki huyo wa pembeni alirudishwa rumande Agosti mwaka jana, lakini aliachiliwa kwa dhamana mwezi Januari.

Alisimamishwa kazi na mabingwa wa EPL City baada ya awali kushtakiwa kwa makosa manne ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono miezi tisa iliyopita.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa