Messi ni Harry Potter wa Soka - Vieri.

Nyota wa Barcelona Lionel Messi ni Harry Potter wa kabumbu, hii ni kwa mujibu wa Christian Vieri.

Messi alitoa asisti kwa Ousmane Dembele kwa ufunguzi wa goli la kwanza katika mchezo wa Champions League dhidi ya Juventus na dakika za majeruhi aliweza kufunga goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya kinda Ansu Fati kufanyiwa madhambi eneo la penati.

Mshindi mara sita wa tuzo ya Ballon d’Or alitenegeza nafasi kwa kupiga pasi tano za mwisho na kuisadia Barcelona kujikamatia alama sita na kuongoza katika kundi G.

Messi ni Harry Potter wa Soka - Vieri.

Vieri, ambaye alishinda Serie A na Juventus mwaka 1996-97 na kuchezea Italy mara 49, amemsifu Messi kwa mchango wake kwenye mchezo wa Jumatano mjini Turin.

“Barcelona yenye maajabu, hakuna gemu ambayo walishinda goli sita saba kirahisi, Walicheza mchezo mzuri,” aliiambia CBS Sports.

“Messi ni mchawi wa soka, ni Harry Potter wa mpira wa miguu na pindi akitundika daruga nitaacha kuangalia soka, sitafanya kazi tena kwenye TV, nitaenda kuangalia Netflix kwa sababu kama akiacha kucheza kutakua hakuna mtu wa kumuangalia.

Ni Christiano Ronaldo pekee katika mashindano ya Champions League ametoa asisti nyingi za magoli (38) kuliko Messi (35) tangu aanze kucheza Champions League mwaka 2004-05.


TSH.160,000,000 KUSHINDANIWA!

Tunazungumzia mkwanja wa Tshs.160,000,000! Kupitia Kasino ya Mtandaonii ya Meridianbet unaweza kuwa milionea wakati wowote.

Kamata Mkwanja wako HAPA

22 Komentara

    Messi hana kazi mbovu

    Jibu

    Messi mnyama akiingia uwanjani hatoki hivi hivi barca wangemuachia sijui ingekuwaje

    Jibu

    Messi anajua soka kwakweli tuache utani kwamwanasoka huyo hanaitendea kaz yake kwaumakini

    Jibu

    Kweli kabisa Messi level nyingineeeee

    Jibu

    Messi yupo vzr

    Jibu

    Messi yupo vizuri sana

    Jibu

    Kwa messi na wwchezaji wengine hawako sawa kila mchezaji ananafasi yake na umuhimu wake na ronaldo anajua na messi pia anauwezo wake na hawawezi kufanana viwango kila mmoja ana uwezo wake

    Jibu

    Kiukweli ukiangalia Messi anapokua uwanjani huyu jamaa fundi sana,basi aje Uingereza nae akichafue

    Jibu

    Messi hanaga kazi mbovu hasa pale anapoingiaga uanjani hakoseagi

    Jibu

    Messi Yuko vizuri anajiamini na kazi yake

    Jibu

    Messi makini sana

    Jibu

    Messi mtu mbad

    Jibu

    Messi Yuko vizuri

    Jibu

    Messi namkubal sana

    Jibu

    Mess yuko vizur sana

    Jibu

    Messi anaweza akawa msaada mkubwa kwa Barca lakini ikumbukwe pia wachezaji wengine wanatakiwa kujitoa kama Messi katika kupata matokeo, Kadri siku zinavyozidi kwenda tunamuona Messi anachoka sasa ni wakati wa vijanakurithi mikoba japo swala hili linaonekana gumu sana kwasasa ndani ya Barca.

    Jibu

    Nilijua tu hii mechi Barca wanshinda

    Jibu

    tutasubiri kuona mbadala wa messi kila mchezaji hana viwango vyake kumzidi mwenzie

    Jibu

    Nakubaliana na ww

    Jibu

    La pruga hamn mtu kwenye soka kama huyu

    Jibu

    Ngoj tuone mbadala huo wa la pluga messi e ndapo Kama hataondoka messi nou camp

    Jibu

    Mess yupo vuzurii

    Jibu

Acha ujumbe