Lionel Messi ameelezea umuhimu wa kupata ushindi na sio swala la kuonesha kiwango baada ya Argentina kucheza mchezo wao wa kufuzu kucheza World Cup kwa kuichapa Ecuador 1-0

Messi kwa mara nyingine alikuwa shujaa kwa timu ya Argentina katika dimba la Buenos Aires siku ya Alhamisi kwa kufunga penati waliyoipata dakika ya 13 kwa mara ya kwanza tangu walipofanya hivyo mwezi Novemba mwaka uliyopita.

Messi: Ushindi Ndiyo Jambo Muhimu Zaidi.
Lionel Messi akishangilia goli dhidi ya Ecuador.

Ratiba ya mchezo wa Argentina kuanza mbio za kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar ilipangwa kutimua vumbi mwezi Machi, lakini kutokana na kuzuka kwa janga la Corona mipango yote ilikatishwa.

Miamba hiyo ya Amerika ya kusini hatimaye walirejea dimbani na kuendeleza rekodi yao ya kutofungwa katika michezo nane waliyocheza na pongezi nyingi zilimuendea nyota na mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or mara sita, Lionel Messi.

“Tulikuwa tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini kitu cha umuhimu ni kwamba tumeshindaa na sasa tunapaswa kuangalia mbele na kufanyia kazi palipo pwaya,” Messi alisema baada ya mechi kuisha.

“Ilikuwa ni muhimu kupata ushindi kwa kuanza sababu tunajua ugumu uliyopo kwa timu zote zinazo taka kufuzu kucheza kombe la dunia.

Messi na wenzake walicheza bila uwepo wa mashabiki katika dimba la La Bombonera kutokana na uwepo wa janga la COVID-19.

Kuna visa zaidi ya 856,000 vilivyoripotiwa mpaka sasa na vifo zaidi ya 22,700 katika taifa la Argentina.

“Ulikuwa ni mwaka mgumu ambao tumeupitia,” alisema Messi wa Barcelona ambaye pia timu yake ya taifa itakutana na Bolivia siku ya Jumanne.


Weka Pesa kwa Airtel Money!

Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!

Soma Zaidi

26 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa