Klabu ya AC Milan ya nchini Italy atakuwa ugenini kukabiliana na Sampdoria ambayo bado anajitafuta toka ligi ianze ikiwa mpaka sasa hajashinda mchezo wowote toka ligi hiyo ya Serie A ianze.

 

Milan Kukabiliana na Sampdoria

Msimu wa Serie A unazidi kuwa wa kusisimua ukiwa na alama nne pekee zikitenganisha klabu nane bora. Mabingwa wa ligi hiyo msimu uliopita AC Milan watasafiri hadi Sampdoria, huku kiongozi wa ligi hiyo  atamkaribisha Cremosense na Napoli atamualika Spezia.

Wakati huo huo Juventus, waliopo katika nafasi ya saba wanatazamia kurejea kutokana na kipigo cha Jumanne kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya, wao watacheza dhidi ya Salernitana. Huku Intermillan wao wakitarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Torino wakiwa uwanja wa nyumbani pale San Siro.

 

Milan Kukabiliana na Sampdoria

Milan bado hajafungwa katika michezo mitano aliyocheza mpaka sasa ambapo ameshinda michezo mitatu na ametoa sare mbili. Kwa upande wa Sampdoria wao ndani ya michezo hiyo mitano amepata sare mbili na amepoteza michezo mitatu huku akishikilia nafasi ya 18 katika msimamo.

Leo hii huu mchezo utakuwa muhimu sana kwa Sampdoria kujitathmini kwani nafasi aliyopo sio nzuri na AC Milan yeye atataka ushindi ili aweze kuendelea kukaa nafasi nzuri na kutetea ubingwa wa Serie A.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa