Mjumbe wa La Liga ukanda wa Tanzania, Rwanda na Burundi Jorge Gazapo leo Septemba 6, 2022 ameweka wazi mipango ya La liga barani Afrika hususani Tanzania na kusema kuwa wamejipanga vizuri katika kuleta mabadiliko kwenye soka.

 

Mipango La Liga Santander Tanzania

Akibainisha hayo kwenye mdahalo na waandishi wa habari za michezo kwenye hotel ya Peninsula Masaki Jijini Dar Es Salaam, alisema kuwa La Liga kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF wamejipanga kuviwezesha vilabu katika kuendelea kimichezo kwa kuwaletea makocha kutoka La Liga, kuzileta timu kucheza na vilabu vya hapa Tanzania.

“Tuna malengo mengi na soka la Tanzania kwa Ushirikiano na TFF, tutakuwa tunawaleta makocha ili kuwafundisha vijana na timu za vijana mfano Chipkizi Cup ktoka Future Youth Academy ya Arusha, tunataka kutoa ushauri wa mfumo wa mabadiliko kama ule wa Yanga SC”

“Lakini pia tupo tayari kushirikiana na vyuo pamoja na taasisi za elimu ili kufundisha soka la kisasa” Alisema Jorge.

Mipango La Liga Santander Tanzania

Mbali na hayo aligusia juu ya uwekezaji mkubwa uliofanya na La Liga kwa ushirikiano na Find Ivestment (CVC), ili kuendeleza mpango wao unaoitwa “Boost La Liga” ambapo, kwenye udhamini huu wenye thamani ya Takribani Euro Bilioni 2.

“Pesa hizi zitagawiwa kwenye vilabu vilivyokubali uwekezaji huu isipokuwa kwa Real Madrid na FC Barcelona, na asilimia 75 itaelekezwa kwenye uboreshwaji wa miundombinu ya klabu, asilimia 15 italipa madeni na asilimia 15 nyingine itatumika katika usajili wa wachezaji”.

Mipango La Liga Santander Tanzania

Akigusia juu ya ubora wa Ligi hiyo duniani alisema kuwa, kwa sasa Ligi hiyo inaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi sana kwenye mitandao ya kijamii kwa jumla ya wafuasi 160M, na jumla ya mitandao 17 tofauti hufuatilia Ligi hiyo na maudhui yanayohusu Laliga huandikwa kwa takribani lugha 20 tofauti.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa