Ndege ya Messi Matatani

  • Lionel Messi alifanya safari 52 kwa ndege yake binafsi ndani ya miezi mitatu msimu wa joto.
  • Ndege ya mshambuliaji huyo ilitoa tani 1,502 za hewa ya Ukaa wakati wa safari
    Ilitoa kiasi sawa na Mfaransa wa kawaida angetoa katika miaka 150.
  • Ushahidi unaonyesha idadi ya safari za kwenda na kutoka Ulaya na Amerika Kusini.
Ndege ya kibinafsi ya Lionel Messi ilitoa hewa ya kaboni ndani ya miezi mitatu tu ikiwa ni sawa na raia wa kawaida wa Ufaransa angetoa hewa hiyo kwa miaka 150, kulingana na ripoti. Ndege hiyo inadaiwa kufanya safari 52 kuanzia Juni 1 hadi Agosti 31.

Kulingana na L’Equipe kupitia Zach Lowy, safari 30 kati ya hizo zilikuwa za mabara na 14 zilivuka Atlantiki, na kusababisha viwango vya juu vya utoaji wa hewa ya ukaa katika miezi mitatu tu.

 

Messi
Mshambuliaji wa PSG-Lionel Messi

Jumla ya uzalishaji wa ndege hiyo katika kipindi cha miezi mitatu ni tani 1,502 za hewa ya ukaa.

Ushahidi unaonyesha mfululizo wa safari kati ya Argentina na Amerika, haswa hadi Miami lakini pia moja ilikuwa ni ya New York. Alisafiri kwa ndege kati ya Buenos Aires nchini Argentina na Miami mara tano kwa jumla.

 

Ndege ya Messi Matatani
Picha ya Ripoti ikionesha safari za ndege binafsi ya Messi

Pia kulikuwa na safari tatu kati ya Montevideo, nchini Uruguay, na Miami, Juni 10, Juni 22 na Juni 23. Pia kuna safari za kwenda na kutoka Brazili, na safari kadhaa za ndege kati ya Ulaya na Amerika Kusini.

Mshambuliaji huyo wa PSG pia alisafiri kwa ndege kwenda au kutoka Barcelona mara saba katika msimu mzima wa Ligue 1. Safari pia zilijumuisha safari za Tenerife, Bilbao, Nice na Figari.

 

Ndege ya Messi Matatani

Habari hizo zinakuja katika wakati wa maonyo kadhaa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa na kuwataka wanadamu kufanya juhudi zaidi kutunza sayari.

Acha ujumbe