KIKAO cha wanachama, viongozi na wadau mbalimbali wa Pan African kilichofanyika jana ndicho kilichounda kamati ya usajili kwa ajili ya timu ya msimu ujao.

Kamati hiyo inaundwa na wajumbe sita ambao walichaguliwa kwenye kikao hicho kilichofanyika katika hoteli ya Falcon iliyopo Lumumba, Dar.

Akizungumza kuhusu uchaguzi wa kamati hiyo Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa “Kikao cha jana kilikuwa maalum kwa ajili ya kupanga mikakati ya msimu ujao.

“Tumechagua wajumbe sita wanaounda kamati ya usajili ambao ni Mwinijuma Kondo, Paul Ambroce Lusozi, Mohamed Mkweche, Nurdin Kisabalala, Omari Dihimbo na Mustafa Wambali.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa