MLINZI wa zamani wa Simba ambaye sasa ni kocha wa timu ya Taifa ya mpira wa ufukweni, Boniface Pawasa ameweka wazi kuwa ukimya mkubwa ambao Simba wamekuwa nao katika suala zima la usajili wao kuelekea msimu ujao, ni mbinu ya kuhakikisha hawapigwi bao na Yanga kwa wachezaji wanaowahitaji.

Simba mpaka sasa wametambulisha nyota mmoja tu, ambaye wamekamilisha usajili wake kuelea msimu ujao ambaye ni kiungo Mzambia, Moses Phiri huku wakiweka wazi kuwa tayari wamekamilisha usajili wa wachezaji wakubwa ambao wamefanya kuwa siri.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa tayari Uongozi wa klabu hiyo imekamilisha usajili wa straika wa Vipers, Cesar Manzoki na Victor Akpan huku wakiendelea kusaka nyota mpya kwa ajili ya kikosi chao.

Akizungumzia ishu ya usajili wa timu hizo mbili, Pawasa alisema: “Unajua kumekuwa na mambo mengi hasa linapokuja suala la usajili ndani ya klabu za Simba na Yanga, kubwa zaidi ikiwa ni ishu ya kuibiana wachezaji ambapo mara nyingi mwenye nguvu ya kiuchumi hushinda.

“Sasa nadhani kwa upande wa Simba wanaonekana kuwa kimya kwa sasa, kwa kuwa wamekuja na mfumo tofauti wa kufanya siri usajili wao ili kuhakikisha Yanga haiwazunguki na kuwaiba.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa