Mahakama ya uhalifu ya shirikisho nchini Uswizi imewaachilia huru viiongozi wa zamani wa FIFA na UEFA Michel Platini na Sepp Blatter kwa mshtaka rushwa yaliyokuwa yanawakabili baada ya kukutwa hawana hatia.

Mwaka jana Blatter na Platini walikuwa wakishtakiwa kwa udanganyifu na makosa mengine na mamlaka ya Uswizi kuhusiana na malipo ya milioni 2 za Uswizi yaliyotolewa na Blatter kwa Platini mwaka 2011.

Blatter alikuwa akishtakiwa kwa udanganyifu, matumizi mabaya ya ofisi na kugushi nyaraka mbalimbali na Platini alikuwa akishtakiwa kwa udanganyifu, matumizi mabaya ya ofisi na kugushi nyaraka pia kushiriki kwenye uhalifu.

Lakini washtakiwa walikana mashtaka yote na mahakama haikuwakuta na hatia na kuachiliwa huru siku ya Ijumaa.

Blatter alipewa CHF 82,000 ili kulipia gharama zake za utetezi wakati kesi ikihunguruma na CHF 20,000 kama fidia. Platini alipokea CHF 143,000.

Blatter alisema: “Sijawahi kuwa mtu mwema kwenye maisha yangu yote lakini kwenye kesi hii mimi ni mwema”.

Platini alielezea furaha yake baada ya kushinda kesi: “Nataka kuelezea furaha niliyonayo kwa wapendwa wangu wote kwamba hatimaye haki imetendeka baada ya miaka saba ya uongo na kunichafua.


BASHIRI HAPA KWA ODDS KUBWA NA MACHAGUO MENGI ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa