Pochettino: Messi Atacheza Popote Anapotaka.

Mshambuliaji Lionel Messi anayetaka kuondoka kunako klabu ya Barcelona “atacheza popote anapotaka” na yupo vizuri kuwa mchezaji bora katika ligi atakayo kwenda, hii ni kwa mujibu wa Mauricio Pochettino.

Messi ameitaarifu Barca hamu yake ya kutaka kuondoka klabuni wiki iliyopita na inaarifiwa kwamba anaweza akaondoka kwa uhamisho huru baada ya kupitia vifungu katika mkataba wake ambavyo vinamruhusu kuvunja mkataba.

Lakini, Barca na LaLiga wanataka malipo yafanyike kama Messi akitaka kuvunja mkataba na dau la €700m litatakiwa kulipwa ili aruhusiwe kuondoka katika klabu hiyo ya LaLiga.

Baba wa nyota huyo wa Argentina ambaye ni wakala wake bwana Jorge Messi amekutana na rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu siku ya Jumatano kwaajili ya mazungumzo kuhusu Messi kuondoka na kuhamia Manchester City klabu iliyoonesha nia ya kumsajili Messi.

Mshambuliaji Lionel Messi

Na Pochettino, ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kuhusishwa kuchukua nafasi ya Setien kabla ya Koeman haja lamba dili ya kuinoa timu hiyo, anatarajia mtaifa mwenzake huyo  aseme neno la mwisho kuhusu hatma yake.

“Lolote linaweza likatokea, Messi anaweza kucheza popote anapotaka ndani ya Spain au Premier League. Yupo tayari kuwa mchezaji bora ligi yoyote,” Pochettino aliiambia Argentine outlet Ole.

Pochettino amekuwa bila timu tangu aondoke Tottenham mwezi Novemba na alikuwa akitizamiwa kutua Camp Nou kufuatia kuondoka kwa Quique Setien mwezi uliyopita.

Mchezaji huyo wa zamani wa Espanyol na kocha wa miaka ya hivi karibuni aliwahi kunukuliwa akisema kwamba “ni bora afanye shughuli za kilimo kuliko kuifundisha Barca.

Siku za hivi karibuni alirudi tena kwenye media na kusema “anajutia usemi wake na hakuwa sahihi kutamka vile sababu huwezi jua nini kitatokea katika maisha.


SHINDA NA HI LO

Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.

Cheza sasa

40 Komentara

    Huyu messi nae siaende anapotaka kwenda tuuu.

    Jibu

    Kazi sasa kwa vilabu kutafuta hilo day la kumfanya Messi kuondoka Barca man city nafasi ndio hii wajitutumue

    Jibu

    messi aende tu kokote kambi

    Jibu

    Haya maneno sasa

    Jibu

    Barca wanatakiwa kuheshimu uamuzi wa Messi kama heshima amewatengenezea heshima kubwa sana kwenye ulimwengu wa soka, now its time for them to be fair enough and see how they will overcome the situation.

    Jibu

    Messi yuko vzuri popote

    Jibu

    Shida co kucheza ishu ni kupaformu timu akayokwenda kucheza na heshimah watakayo mpa je itafikaha kama ya nou camp au argentina ngoj tuone movie hiii itakwisha je

    Jibu

    Kweli kabisa wasimpangie

    Jibu

    Mwacheni aende anapoona panamfaa.

    Jibu

    Messi nenda popote tu unapotaka kwan kambi popote#Meridianbettz

    Jibu

    Messi nae anatuchangany kokote kambi si aende anapotaka yy!!

    Jibu

    itakuwa vizuri sana messi wamuache tu aondoke barcelona akalete ushindani ligi nyingine

    Jibu

    Maisha yanaenda kasi sana

    Jibu

    Messi namkubali sana

    Jibu

    Messi unakwama wapi kokote kambi mzee

    Jibu

    Maamuzi ni yake popote anaweza kwenda kucheza

    Jibu

    Nikweli kabisa Pochettino anacho kisema Messi atacheza anapo pataka yeye uwamuzi niwake yeye Kama yeye Messi

    Jibu

    aya ndo mambo niliyokua nataka kuyasikia

    Jibu

    Safi sana messi nimeipenda mnoo

    Jibu

    Maamuzi ni yake mwenyewe

    Jibu

    Kwa umri wake naona anatafuta pa kumalizia mpila wake tu

    Jibu

    Sawa afanye tu anavyotaka

    Jibu

    Ni maamuzi yake mwenyewe

    Jibu

    Afanye chaguo mwenyewe,wapi panamfaa kuendeleza kandanda!!

    Jibu

    Messi jeshii yuko vizur

    Jibu

    Messi ni mchezaji mzuri popote anacheza

    Jibu

    Maoni: kiukweli kwa uwezo wa messi anaweza kucheza timu yoyote ile hata akija yanga freshi tu.

    Jibu

    Yuko sahihi

    Jibu

    Yuko sahihi sidhani Kama kuna timu duniani kote itakua haimuhitaji messi la! hasha.

    Jibu

    Barcelona inaonekana kuwa bado wanataka mana sio kwa sheria hiyo ambayo wameweka ya kuvunja mkataba kwa hela hiyo mana wanajua kuwa uchumi umeshuka sana na isitoshe lion messi ni mchezaji ambaye anajua anacho kifanya .ndiyo mana wameweka hivyo ili kumkomoa tu wamuache tu aondoke kuliko kumpotezea mda tu

    Jibu

    Yuko sahihi kabisah asemavyo kocha wa Spurs

    Jibu

    Ni kweli messi hana uwezo was kwenda kuchezea maali popote ila kwa mahamuzi yake ya sasa sio sahihi kwa clabu ya Barcelona ukiangalia kabic bado wanaumimu nae

    Jibu

    Messi maamuzi Ni yake mwenyewe
    @meridianbettz

    Jibu

    Uwamuzi niwake

    Jibu

    Mess kuondoka barca ni swala gumu kwa kuwa barca haitawwz kumruhus kirahis itabid timu inayomsajil imwage mpunga mrefu

    Jibu

    Messi ni kama dhahabu jinsi ilivyopendwa na kila mtu#meridianbettz

    Jibu

    Hebu mpumzshen kdogo afanye anachotaka bas

    Jibu

    Messi kama heshima amewatengenezea heshima kubwa sana kwenye ulimwengu wa soka

    Jibu

    Kwer afanye maamuz yake hasichanganywe watu

    Jibu

    Messi Mwoga sana Hawezi toka Barca

    Jibu

Acha ujumbe