BAO pekee la Oscar Paul dhidi ya JKT Tanzania ndilo lililowapa Tanzania Prisons ujeuri wa kuendelea kubaki kwenye michuano ya Ligi Kuu kwa msimu ujao.

Mchezo huo wa mtoano ‘plaoff’ uliopigwa leo jumamosi kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo ni wa kwanza huku timu hizo zikibakiwa na dakika 90 za kujua hatma yao.

Bao hilo pekee katika mchezo huo lilifungwa dakika ya 37 ya mchezo huo huku ule wa marudiano unatarajiwa kupigwa wikiendi ijayo kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa