Aliyekuwa kocha wa muda wa Manchester United Ralf Rangnick amesema hataendelea na kazi yake ya Ushauri katika Klabu ya Manchester United na sasa anaelekeza nguvu zake kuinoa timu ya Taifa ya Soka ya Austria

Rangnick amekuwa Kocha wa muda wa Man. United baada ya kufukuzwa kwa Kocha Ole Gunnar Solskjaer na ameiwezesha timu hiyo kumaliza katika nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu ya England

Baada ya kumaliza kuwa Kocha wa muda na kuteuliwa kwa Kocha Erik ten Hag, Rangnick alitakiwa kuwa Mshauri wa Timu hiyo ya Old Trafford, lakini sasa Klabu imethibitisha haitakuwa hivyo.

Rangnick alithibitisha habari hizo katika mkutano na waandishi wa habari na Austria Jumapili na Manchester United ilisema:

“Tungependa kumshukuru Ralf Rangnick kwa juhudi zake kama meneja wa muda katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

“Kwa makubaliano ya pande zote mbili, Ralf sasa atazingatia tu jukumu lake jipya kama meneja wa timu ya taifa ya Austria na kwa hivyo hatachukua nafasi ya ushauri huko Old Trafford.

“Tungependa kumtakia Ralf mafanikio mema katika sura hii inayofuata ya kazi yake.”


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa