Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Raphinha hajaziondoa tetesi za yeye kuondoka Leeds wakati wa dirisha hili la usajili na inaripotiwa Barcelona wanahitaji saini ya mchezaji huyo.

Raphinha: Bado Nina Mkataba na Leeds Lakini Acha Tuone

Winga huyo mwenye umri wa miaka 25 alitua Leeds mwaka 2020 akitokea Rennes ya Ligue 1 alifunga mabao 11 na kuisadia Leeds kuepuka kushuka daraja msimu uliyopita.

Raphinha amesaliwa na miaka miwili kwenye mkataba wake na Leeds akiwa yupo kwenye majukumu na timu ya taifa alisema hana uhakika ni wapi atakuwa mpaka mwisho wa dirisha la usajili.

“Nina mkataba na Leeds mpaka mwaka 2024  kwa hiyo hatima yangu ipo mikononi mwa Deco na Leeds,” alisema

“Akili yangu sasa ipo na timu ya Taifa kwa michezo inayokuja pia nipo kwenye mapumziko kwa sasa.

“Kama nisalia au nitaondoka sawa lakini nitaonyesha uwezo wangu na kuangalia fursa na kujaribu wakati wa michuano ya kombe la Dunia.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa