Mchezaji wa timu ya Tottenham Hot Spurs Richarlison ametokwa na machozi ya furaha hapo jana baada ya kufunga mabao mawili yaliyofanya Spurs aondoke na alama tatu katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

 

Richarlison Atokwa na Machozi

Richarlison amepachika mabao hayo wakiwa nyumbani kwao ambapo waliwaalika Marseille katika mechi yao ya kwanza huku mchezaji huyu ikiwa hayo ni mabao yake ya kwanza kufunga toka ajiunge na klabu hiyo msimu huu.

Mchezaji huyo ametokwa na machozi ya furaha baada ya kuiona familia yake ambayo ilikuja kumpongeza kwa kufanikiwa kufunga mabao hayo huku ikiwa ni msimu mwingine wa Spurs kushiriki michuano hii baada ya kutoshiriki msimu uliopita.

 

Richarlison Atokwa na Machozi

Mabao hayo ya Richarlison yalifungwa katika kipindi cha pili ambao timu hiyo ya Marseille inayocheza Ligue 1 ya Ufaransa kupata adhabu ya kadi nyekundu  hivyo ikiawa ni ngumu kwao kuzuia mashambulizi ya vijana wa Antonio Conte.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa