Ricky Hatton Afikisha Miaka 9 Tangu Astaafu Ndondi.

Bingwa wa zamani wa dunia na bondia wa Uingereza, Ricky Hatton siku kama ya leo mwaka 2011 alitangaza kuachana na mchezo wa Masumbwi.

Mwanandondi huyo aliyestaafu mwaka wa 2011, ambaye kwa sasa ni mkufunzi wa mabondia, kuna wakati alieleza kuwa alishawahi kujaribu kujiua.

“Nilijaribu kujiua mara kadhaa,” alisema. “Nilikuwa nikienda kwenye baa, kurudi, nikilia kwenye giza nikiwa nimetoa kisu.” “Mwishowe nilihisi kuwa huenda nikajiuwa kwa kulewa kwa sababu nilikuwa na uchungu mwingi.”

Hatton ameiambia BBC kuwa kuna umuhimu wa mabondia kupewa ushauri na kusaidiwa wanapostaafu ili kupata nafuu kutoka kwa shinikizo za akili.

“Wanasoka wana maajenti na wasimamizi wanaowasaidia katika vilabu vyao, lakini mabondia, mara tu muda wao unapoisha, unabaki peke yako,” alimaliza.

“Kuna mengi yanayofaa kufanywa kuwasaidia mabondia, wengi wetu tanaathirika kwasababu huu mchezo mtu yuko pekee yake na unapostaafu, unaishi maisha ya upweke”.

Hatton alipokonywa kibali cha ndondi mwaka wa 2010 baada ya kukiri kutumia mihadarati aina ya ‘Cocaine’.

Aidha, ameshinda mapigano 21 yakiwemo kumcharaza bingwa wa dunia wa light-welterweight Kostya Tszyu mjini Manchester mwaka wa 2005 na kuondoka na taji la IBF.

Mwaka wa 2006 alitangazwa bingwa wa dunia wa WBA.

Hata hivyo alikomeshwa na Floyd Mayweather Jr mnamo mwezi Disemba 2007 na Manny Pacquiao mwezi Mei mwaka wa 2009.

51 Komentara

    Alikuwa bondia saf san

    Jibu

    Ricky alikuwa bondia mwenye kipaji kizuri

    Jibu

    Maoni:daah mwamba alikuwa noma

    Jibu

    Ngumi msumari nouma Sana meridianbettz

    Jibu

    Alikua anajua

    Jibu

    Asante update#meridianbettz

    Jibu

    Kwa Ricky ni bondia ambaye usingetamani astaafu mapema

    Jibu

    Aiseee pole sana

    Jibu

    Haya Mamichezo nayo sio ya kupigana mda mrefu#Meridianbettz

    Jibu

    Alikuwa bondia bora namkubali sana

    Jibu

    Alikuwa bondia mwenye mfano wa kuigwa

    Jibu

    Bondia mahir

    Jibu

    Yuko sahihi sana Ricky Hatton kuacha peke yako katika soka la ngumi inatokea sana hasa kwa watu ambao ni maarufu ususani michezo unapo staafu unakuwa kila kitu umemaliza kama hukuweza kujiwekea msingi mapema kabla hujastaafu basi huwezi kuwa wa dhamani kwao na kukusahau kama ulikuwa unadhamini kwao katika uchumi .hivyo sio ngumi tu hata watu wanao Fanya kazi serikalini huwa wakistaafu wanakuwa wapeke hivyoabadiliko sijui yataaza lini .asante meridianbettz kwa nakala nzuri.

    Jibu

    Bondia yuko vizur

    Jibu

    Bingwa wa zamani wa dunia na bondia wa uingereza

    Jibu

    Kaacha bonge la historia

    Jibu

    Miaka inaenda,Ricky alikua bora hata kwenye ufundishaji wake utakuwa bora

    Jibu

    Alikuwa bondia poa sana

    Jibu

    Alikuwa mahili Sana katika ngumi

    Jibu

    Jamaa bado uwezo Alikuwa nao ,Yani anastafu kiwango chake Kama ataamua kurudi bado atakinukisha tu

    Jibu

    Jamaa alikuwa noma sana

    Jibu

    Mashabiki wa ndondi watamkumbuka sana

    Jibu

    Namkubali sana bondia hiyi

    Jibu

    Alikuwaga bondia mzuri wa ngumi

    Jibu

    Namkubali sana uyu bondia Alikua vizuri

    Jibu

    Kumbe Halton alikua kisiki kwenye uzito wa Kati duniani anastahili pongezi ila wengi wao wanakua wakijikita kwenye madawa wa kulevya.

    Jibu

    Bondia mahili na mwenye kujituma akiwa ulingoni

    Jibu

    Kaacha bonge la historia

    Jibu

    Hiyo nibonge ya historia

    Jibu

    Amekuwa mpambanaji sana hongera yake#meridiznbett

    Jibu

    Ana rekodi nzuri

    Jibu

    Ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Ricky alikuwa anajua ngum#meridianbettz

    Jibu

    Ricky alikua balaaa sanaa

    Jibu

    Mwanandondi huyo aliyestaafu mwaka wa 2012, ambaye kwa sasa ni mkufunzi wa mabondia, alieleza kuwa amepitia uchungu mwingi namfaham sana 👍 na nakumbuka alishawai kusema
    “Nilijaribu kujiua mara kadhaa,” alisema. “Nilikuwa nikienda kwenye baa, kurudi, nikilia kwenye giza nikiwa nimetoa kisu.” “Mwishowe nilihisi kuwa huenda nikajiuwa kwa kulewa kwa sababu nilikuwa na uchungu mwingi”.
    Hatton ameiambia BBC kuwa kuna umuhimu wa mabondia kupewa ushauri na kusaidiwa wanapostaafu ili kupata nafuu kutoka kwa shinikizo za akili.
    “Wanasoka wana maajenti na wasimamizi wanaowasaidia katika vilabu vyao, lakini mabondia, mara tu muda wao unapoisha, unabaki peke yako,” alimaliza.
    anasema kuwa alijaribu kujiua mara kadhaa kutokana na tatizo la shinikizo la kiakili
    “Kuna mengi yanayofaa kufanywa kuwasaidia mabondia, wengi wetu tanaathirika kwasababu huu mchezo mtu yuko pekee yake na unapostaafu, unaishi maisha ya upweke”.
    Hatton alipokonywa kibali cha ndondi mwaka wa 2010 baada ya kukiri kutumia mihadarati aina ya ‘Cocaine’.
    Aidha, ameshinda mapigano 21 yakiwemo kumcharaza bingwa wa dunia wa light-welterweight Kostya Tszyu mjini Manchester mwaka wa 2005 na kuondoka na taji la IBF.
    Mwaka wa 2006 alitangazwa bingwa wa dunia wa WBA.
    Hata hivyo alikomeshwa na Floyd Mayweather Jr mnamo mwezi Disemba 2007 na Manny Pacquiao mwezi Mei mwaka wa 2009.

    Jibu

    Kuna mengi yanayofaa kufanywa kuwasaidia mabondia, wengi wetu tanaathirika kwasababu huu mchezo mtu yuko pekee yake na unapostaafu, unaishi maisha ya upweke #meridianbettz

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    inabidi sasa aendeleze vipaji vya mabondia zaid

    Jibu

    Bondia hatar

    Jibu

    Mwamba champion atakumbukw kwa mengi

    Jibu

    Duh kweli ngumu ni ngumutu…

    Jibu

    asante sana kwa update

    Jibu

    Hongera Sana Ricky hatton kwa kuacha historia nzuri ya ndondi

    Jibu

    Alikua hatar sana

    Jibu

    Duu mzee wa ngumi jiwe maana wanapo staafu hawa wacheza masumbwi wanapa ugongwa wa akili muda flan

    Jibu

    Maoni:jamaa alikua noma sana kwenye ngumi

    Jibu

    Duu safii mzee wangumi yupo vizuri yupo Kama ajastaafu kweli Anastairi pongez zake

    Jibu

    Masumbwi sio pouwa

    Jibu

    Ngumi nazo muda mwingine sio nzuri.

    Jibu

    Maoni:Ni bondia mwenye rekodi nzuri sana

    Jibu

    Madawa ndiyo yamechangia kumtoa mchezoni.

    Jibu

Acha ujumbe