Mwaka 2019 Rodrygo alipiga chini nafasi ya kuijunga na Barcelona na badala yake alijiunga na Real Madrid kipindi ambacho aliondoka Santos.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 21 alikuwa mchezaji muhimu katika msimu uliyoisha ambapo Real Madrid walitwaa mataji ya LaLiga na Ligi ya Mabingwa akiwa amefunga mabao manne na kusaidia mengine manne.
Barca walihitaji saini yake miaka mitatu iliyopita, Rodrygo alisema baba yake hakuamini alipokataa Blaugrana, na alimwambia: “Unatarajia nini? Utacheza na Lionel Messi!”
Lakini hatimaye mambo yalienda vyema kwa mshambuliaji huyo, ambaye pia ameingia kwenye kikosi cha Brazil na anaonekana yuko katika nafasi nzuri ya kuchezea taifa lake kwenye Kombe la Dunia la Qatar baadaye mwaka huu.
“Nilirudi nyumbani baada ya mchezo nilikuwa na jezi ya Real Madrid nyumbani kwangu na baba yangu aliingia chumbani kwangu akiwa amevaa jezi hiyo na nyingine ya Barcelona.
“Aliniambia, ‘sasa chagua’… na nikachagua moja ya Real Madrid.”
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.