Ronald Koeman: Hatuwaogopi PSG!

Hispania; Barcelona wamepangwa kucheza na mabingwa wa Ufaransa Paris Saint-Germain katika hatua ya mtoano ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa. Ronald Koeman ana lipi hapa?

Bosi wa Barcelona, Ronald Koeman anasema kuwa wao wanawaheshimu sana PSG lakini hawaogopi kukutana nao kwenye gemu anayoitaja kuwa itakuwa “Nzuri” sana.

Mechi yao ya kwanza itachezwa mnamo Februari 16 huko Camp Nou kabla ya mchezo wa marudiano huko Paris ambao utakuwa Machi 10.

PSG ilifikia hatua fainali ya michuano hii msimu uliopita ila walikwama mbele ya mabingwa Bayern Munich, lakini wamebarikiwa na talanta za washambuliaji wenye uwezo mkubwa wakiwemo Neymar Junior na Kylian Mbappe.

Ronald Koeman
Ronald Koeman

Neymar ni mchezaji wa zamani wa Barcelona, ​​ameshinda Ligi ya Mabingwa na Barca huko nyuma mnamo 2015. Kwa sasa anauguza jeraha lakini anatarajiwa kurejea kuwa shwari wakati wa kukabiliana na klabu yake ya zamani.

Mbappe anachukuliwa kama moja ya chipukizi machachari zaidi kwenye soka la Ulaya na amehusishwa sana na kuhamia Real Madrid msimu huu wa joto.

Ronald Koeman, baada ya matokeo ya droo ya Ligi ya Mabingwa anasema kuwa alitambua kuwa wangecheza moja ya timu kubwa, yenye nguvu.

“PSG ni timu yenye nguvu, lakini pia ni ngumu kwao kwa sababu sisi pia ni timu ngumu na naona ni sawa kabisa.” Ronald Koeman

“Katika miaka ya hivi karibuni wametumia pesa nyingi kuijenga timu ambayo inaweza kupigania mataji makubwa kama Ligi ya Mabingwa. Msimu uliopita walifika fainali, na ni timu ambayo itaendelea kuwepo”

Koeman anaamini kuwa, licha ya kuwa na nguvu, PSG lazima wajue kuwa wanaenda kukutana na Barcelon ambao ni wagumu pia. Matarajio yake ni kuwa mechi zote zitakuwa nguvu, lakini watajitahidi kushinda.


 

BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

11 Komentara

    Ni vizuri kujiamini koeman anajua nini anafanya

    Jibu

    Mpira dk 90

    Jibu

    Ngoja tuone

    Jibu

    Vizuri kujiamini ndio kitu kizuri

    Jibu

    Barca wapambane

    Jibu

    Kapgen kaz achen maneno

    Jibu

    Psg wanaonekana wapo kwenye kiwango Bora zaidi ya vijana wa Koeman nadhani anatakiwa kujidhatiti lakini sio kuongea kuwa hawawaogopi PSG.

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Koeman kesha anza woga

    Jibu

Acha ujumbe