Nyota wa Manchester United Cristiano Ronaldo amekuwa akishambuliwa kwa maneno na watu wengi ambao hawajafurahishwa na kitendo alichofanya na kusababisha simu ya shabiki mmoja kuanguka baada ya mechi ya juzi kati ya Manchester United na Everton.
Mlinzi wa zamani wa Liverpool Jose Enrique (36) ametoa maoni yake ya wazi kuhusu Ronaldo ambaye ameshawahi kucheza naye wakati akiwa katika ligi ya England. Jose ametangaza “simpendi, siku zote nimesema , simpendi, anaamini kuwa yeye ni Mungu na anaweza kufanya lolote analotaka,”

Jose aliandika hayo kwenye mtandao wa Instagram juu ya video iliyoonyesha kitendo alichokifanya Ronaldo jumamosi iliyopita.
Mwanasoka huyo mwenye asili ya Hispania hakuishia hapo , aliendelea kwa kusema kuwa mtazamo wake kuhusu Ronaldo unatokana na utu na sio uwezo wake. “Hii haibadilishi kuwa yeye ni mmoja wa wachezaji bora kuwahi kutokea katika historia ya soka lakini yeye kama mtu ,simpendi”.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.