Polisi wa Merseyside wamefungua jarada la uchunguzi kufuatia kitendo cha mchezaji nyota wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo akionekana akiputa simu ya shabiki wa klabu ya Everton kwenye mchezo ambao Man Utd walipoteza kwa goli 1-0.

Baada ya video yake akiwa anaputa simu ya shabiki kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Mchezaji huyo nyota wa United Ronaldo nae alitumia ukarasa wake kwenye mtandao wa kijamii kuomba radhi kwa kufanya kitendo hicho na kumualika shabiki kuangalia mchezo kwenye dimba la Old Trafford kama ishara ya fair play na unamichezo.

Ronaldo
Cristiano Ronaldo

msemaji wa polisi wa Merseyside alinukuliwa akisema , “tunaweza thibitisha kwamba tuko kwenye mazungumzo na manchester united na Evertin kufuatiwa tuhuma za shambulio kwenye mchezo wa Everton vs Man Utd kwenye dimba la Goodison park.

“Ikiwa wachezaji walikuwa wanatoka saa 2.30pm, iltolewa taarifa kwamba kuna kijana alishambuliwa na moja ya timu ya ugenini wakati wakiwa wanaotoka uwanjani.

“Maelezo bado yanashughulikiwa na maofisa  kwa sasa wanafanya kazi na klabu ya Everton kupitia ccctv kamera na kufanya uchunguzi wa nguvu ili kupata ushaidi kama kuna kosa lolote la kuchukuliwa hatua”

Klabu ya Manchester United walithibitisha kuwa wanatambua jambo hilo, msemaji wa klabu alitoa waraka uliosema. “Tunatambua shutuma za ajari hiyo baada ya mchezo wa leo kuisha, sisi na everton tutashirikiana na everto kutoa maelezo yoyote yatakayohitajika.”


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa