Mchezaji wa zamani wa Manchester United Wayne Rooney amekubaliana na klabu ya D.C. United ya MLS na tayari amerejea nchini Marekani kwaajili ya kuanza majukumu mapya na klabu hiyo.

Rooney Kurejea Ligi ya MLS Kama Kocha wa D.C United

Rooney (36) ambaye alikuwa kocha mkuu wa klabu ya Count Derby kunako Championship msimu uliyoisha aliwahi pia kucheza katika ligi kuu ya Marekani miaka ya 2018 na 2019 na sasa anakwenda kuchukua nafasi ya kocha wa muda wa D.C. United Chad Ashton ambaye alipewa dili hilo baada ya kutimuliwa kwa kcoha Hernan Losada.

Kwa sasa timu ya D.C. United imeketi katika nafasi ya pili mwishoni wakiwa wamekusanya pointi 17 katika Easter Conference MLS baada ya kukosa nafasi ya mchujo kwa misimu miwili mfululizo.

Kwa mujibu wa taarifa Rooney amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles siku ya Jumapili mchana kwaajili ya kuungana na D.C. United na kukamilisha taratibu za kusaini mkataba. Je Rooney ataleta mabadiliko kwenye kikosi cha D.C United.


CHEZA KASINO HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa