Shaffih Dauda : Hatuna Jitihada , Si Mara ya Kwanza Kua wa 3

Shaffih Dauda Moja ya watangazaji na wachambuzi nguli wa michezo tanzania mapema leo amepost kwenye kurasa wake wa mtandandao wa kijamii Instagram kwa kuandika maneno yenye lengo la kujenga namna nzuri ya kuisogeza timu yetu ta Taifa kufikia malengo.

“Kwanza tukubali nafasi ambayo tumemaliza kwenye Kundi letu tumestahili kuwa katika nafasi hiyo [nafasi ya tatu kwenye Kundi J tukiwa na alama nane”

“Ni mara kadhaa sasa tumemaliza katika nafasi kama hiyo tukiwa na alama kama hizo katika michakato ya kufuzu kwenda kwenye mashindano makubwa. Hii inaonesha hatujafanya jidihada za makusudi ili kutoka kwenye nafasi tuliyozoea kuishia kwenda juu zaidi.”

Shaffih Dauda

Shaffih dauda pia alisistiza kwa kusema “Inawezekana pia wakati sisi tunapambana kukwenda juu, wenzetu tunaoshindananao wameweka jitihada za kuhakikisha wanakwenda juu zaidi. Kwa hiyo jitihada zetu ziwe na tija kuna mambo mawili, tunaoshindananao washuke ubora au jitihada zetu ziwe kubwa mara dufu kuliko wao.”

Kwa kumalizia ujumbe wake bwana Shaffih Dauda ameacha swali ambalo majibu yake unaweza kuacha kwenye koment ya makala hii .
“Ni ngumu sana kulaumu lakini vilevile ni ngumu kusifia ila naamini kama nchi kuna kitu tumejifunza! Kuna swali tunapaswa kujiuliza kwa nini miaka yote Ghana, Cameroon, Senegal, Mali, Ivory Coast na mataifa mengine ndio yanafuzu lakini sio sisi?”


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe