WAKIENDELEA kuwatambulisha wachezaji wao klabu ya Simba leo jumapili imemtambulisha kiungo Mnigeria, Victor Akpan.
Kiungo huyo ambaye alikuwa akikitumikia kikosi cha Coastal Union kwa msimu uliopita alionyesha kiwango bora kiasi cha kuwashawishi mabosi wa Simba.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa “Kiungo wa kati kati ya dimba mwenye uwezo wa kuhimili mechi za aina zote, Victor Akpan ni Mnyama”
Akpan amesajiliwa ndani ya klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa