Sitaki Kuwa Madrid Kwa Miaka 20 - Zidane.

Zinedine Zidane amesema kwamba hatokaa Real Madrid kwa kipindi kirefu na anatarajia  kustaafu mapema kuliko vile inavyo dhaniwa.

Zidane amekua na matokeo chanya hapo Los Blancos, kwa miaka mitano aliyo itumia akiwa kama mchezaji na sasa akihudumu kama kocha.

Wakati alipo anza kuinoa Madrid kwa mara ya kwanza aliipatia mafanikio ya kihistoria kwa kuweza kunyakua taji la klabu bingwa Ulaya mara tatu mfululizo, ingawa aliondoka mapema,mara baada ya kushinda taji la tatu, alirudi tena mwaka uliyopita kufuatia Madrid kutofanya vizuri chini ya Satiago Solari.

Amerudi Los Blancos akiwa na moto kwa mara nyingine akiwa analiwinda taji la La liga wakichuana vikali na Mahasimu wao kutoka Katalunya Fc Barcelona wakiwa wanafanana pointi lakini Madrid wapo nafasi ya kwanza kwa faida ya kushinda mechi walizokutana.

Lakini ni nadra kwa Zidane kufanya ukocha kwa kipindi kirefu, kwani hata kipindi alipokuwa hajishughulishi na kazi hiyo alikuwa akifanya kazi nyingine tu nchini kwake Ufaransa.

Ikiwa anaelekea kukutana na timu ya iliyo nafasi ya mwisho katika msimamo Espanyol, ambayo imemfukuza kocha wake Abelardo mapema,Zidane  alizungumzia malengo yake ya baadaye pia aliulizwa kuhusu Ramos.

Alipo ulizwa kama Ramos anaweza kuweka alama katika klabu akiwa anacheza kama beki wa kati, alijibu anaweza kufanikisha, sababu ana kiwango kizuri akiwa kama mchezaji na maisha yake kwa ujumla.

“Mara zote amekuwa akitaka ushindi na kuweka historia katika klabu,si shangazwi na akifanyacho, ni bahati kuwa naye katika klabu ya Madrid nadhani ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapo staafu. Siendi kufundisha kwa miaka 20 nitastaafu muda si mrefu, chochote kinaweza kutokea.”

Aliongeza:  “Nilikuwa mchezaji mzuri sana kuliko ukocha, lakini kulikuwa na wachezaji wazuri zaidi yang, ingawa nina furahia kwa nilicho kifanya kwenye soka.”

“Sitafundisha kwa kipindi cha miaka 20,sijui kwa muda gani, sijapanga chochote nafikiria kufanya mambo mengine.

 

47 Komentara

    Sio mbaya kwa kwa uamuzi alioufikiria yeye

    Jibu

    Safi lazma aweke na mda wakupunzk sio mpila t kila ck

    Jibu

    Kazi na umri pumzika tu upishe kipaji kingine

    Jibu

    Asante kwa taarifa#meridianbettz

    Jibu

    Zidane bado nikijana kabisa kwny orodha y makocha hivyo asionyeshe kuchoka mapema kwan kuitumikia club kubwa Kama hiyo n fahar sana kwake
    # meridianbet Tanzania

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    Mzee amechafuka sawa baba tumekuelewa kila la kheri huko uendako kapumzike salama baba

    Jibu

    Uko sahii,mana kufundisha mpira sio kazi raisi.

    Jibu

    Zidane ni kocha mzuri Sana pia amefundisha Madrid kwa muda mrefu Sana na ameiendesha klabu ya Real Madrid vizuri na kutwaa ubingwa mara nyingi sio mbaya akipumzika kufundisha timu ya Madrid kutokana na umri pia umeenda inabidi hastaafu tyuu

    Jibu

    Zidane mjanja Anataka kustaafu kwa Heshima #Meridianbettz

    Jibu

    Zidane kocha bora anetumia akili nyingi na kuwafanya bahadhi ya wachezaji wamepata mafanikio kupitia yeye na kuweka historian katika timu hivyo bado anauwezo wa kuendelea kuwa kocha bado real Madrid wanamuhitaji ingawaaamuzi bado ni yake kubaki au kuondoka

    Jibu

    Zidane ni kocha mchanga sana na kuifundisha timu kama real madrid ni bahati sana kwa heshima ya klabu imempa nafasi hyo kama regindali wa zamani wa timu kocha mdogo timu kubwa

    Jibu

    Maamuzi mazuri

    Jibu

    Makala nzuri sanaaa

    Jibu

    Thnks meridian bet tz kwa update za michezo na burudani

    Jibu

    daah kwanini tena zidane madrid itapwaya bhna

    Jibu

    Zidane mbona kama unatutenga ivi

    Jibu

    Ni uamuz wake mm nitapngaje

    Jibu

    Kwanza zidane mjanja sana anataka kustaafu bila kualibu rekodi yake ya kufundisha mpira anataka kuondoka kabla mambo hayaja halibika

    Jibu

    mzee anapima upepo tu

    Jibu

    Kazi yake ni kufundisha soka ,ni kweli hawezi kuka pale kwa muda mrefu sababu anaweza akatakiwa na timu nyingine akawnda kufundisha

    Jibu

    Uwenda plan zake hataki kuzeekea hapo

    Jibu

    Jamani zidane bado yuko vizuri apige kazi.

    Jibu

    Ametumia maamuzi mazuri

    Jibu

    Uamuz sio mbaya

    Jibu

    Safi tu uamuzi ni wake

    Jibu

    Kweli kabisa.afanye maamuzi tu

    Jibu

    Safi sana inabidi astaagu tuu awaachie na wengine

    Jibu

    Jamani Zidane mbona uko vema kwenye ufundishaji mpira

    Jibu

    Sio mabaya maamuzi yake zidane ameitoa timu ya madrid mbali sana Ni mda wa kustaafu sasa

    Jibu

    Zidane usituache ivy jamani real bado tuna kuhitaji

    Jibu

    Zidane bado kijana hivyo asioneshe kuchoka mapema pia kufundisha clabu kama madrid ni bahati kubwa sana

    Jibu

    safi habar njema

    Jibu

    Zinedine zidane ameshachoka

    Jibu

    Uamuzi mzuri

    Jibu

    Zinedine zidane hata hivyo umli umenda kwa sasa uwamzi wake mzuri

    Jibu

    Sikufurahia kabisa alipostaafu soka mapema , anatakiwa kuendelea kutoa mchango wake katika Ulimwengu wa Soka#meridianbettz

    Jibu

    Angebaki ili alete chachu kwwnye soka kustaafu mapema haijakaa sawa

    Jibu

    Makala mazur

    Jibu

    Hakuna chenye mwanzo kisichokua na mwisho

    Jibu

    Maoni:Zinadine mbona anastaafu mapema alafu soka bado linamuhitaji inabidi afikilie huu uwamuzi wake.

    Jibu

    Kiukweli kazi ya ukocha ni ngumu Sana kocha anapopata mafanikio makubwa katika clubu anastahili pongezi Sana maana anafanya kazi ambayo ni vigumu Sana kupumzisha kichwa

    Jibu

    Maoni:makala nzuri sana

    Jibu

    Yuko sahihi kwa maana kufundisha mpira sio kazi rahisi

    Jibu

    Maamuzi yake hatuwezi kuyapinga Kama kashaamua kusepa sawa achape lapa

    Jibu

    Ni vema kistaafu mapema ukiwa bado akili haijachoka

    Jibu

    Ni bora lakin

    Jibu

Acha ujumbe