Suarez Aanza na Goli 2 na Asisti 1 Akiwa Atletico.

Diego Simeone amevutiwa na kasi aliyoanza nayo Luis Suarez na amevutiwa zaidi na asisti aliyotoa kuliko goli mbili alizofunga kwenye ushindi wa 6-1 dhidi ya Granada siku ya Jumapili.

Suarez aliingia kipindi cha pili dakika ya 70 ya mchezo na ndio ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na Atletico Madrid na aliweka wavuni goli mbili na kumtengenezea asisti mchezaji mwenzake Marcos Llorente.

Mchezaji huyo ambaye ni mtaifa wa Uruguay alijiunga na klabu ya Atletico Madrid kwa dau la €6m akitokea klabu ya Barcelona, katika mchezo wa jana alifanikiwa kutengeneza penati ambayo VAR iliikataa.

Suarez Aanza na Goli 2 na Asisti 1 Akiwa Atletico.
Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Luis Suarez.

Suarez alifunga magoli mawili, moja alifunga kwa kichwa na lingine alifunga baada ya kupiga shuti lililogonga mwamba na kukutana nao tena kisha akamalizia lakini kocha mkuu wa Atletico amekiri kuipenda zaidi asisti aliyompa Llorente aliyetokea benchi.

“Magoli yake mawili ni ya kawaida kwangu mimi lakini ile asisti ni nzuri sana,” Simeone alisema baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.

Diego Costa, Joao Felix na Angel Correa walifunga katika mchezo huo uliyo malizika kwa Atletico kuibuka na ushindi mnono wa 6-1 katika dimba la Wanda Metropolitano na kuweka rekodi ya kushinda kwa goli nyingi katika mchezo wa ufunguzi wakiwa chini ya Diego Simeone.

Atletico watawabana mahasimu wao Real Madrid na Barcelona msimu huu na Simeone anaimani ushindani utakuwa mkubwa baada kila timu kujiandaa vizuri.

“Itategemea kutokana na kazi yetu, Ujio wa Suarez umeongeza chachu ndani ya kikosi chetu na kama wachezaji wote 23 watazithamini dakika za kucheza hakika tutashinda vizuri.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

41 Komentara

    habar njema

    Jibu

    suarez yupo makini sana

    Jibu

    Suarez mwamba

    Jibu

    Deal done 👍

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Suarez Yuko vizuri

    Jibu

    Safi sana kijana mwazo mzuri

    Jibu

    Namkubali Sana Suarez mzee wakutikisa nyavu akoseagi

    Jibu

    Siku zote Suarez ni bora sema barcelona hawakutaka kumpa mda

    Jibu

    hongera zaKE

    Jibu

    Suarez atafanya mengi San pale A.madrid

    Jibu

    Suarez anajua wajibu wake kwenye soka

    Jibu

    Suarez ni mmoja ya mafowadi hatari Sana duniani

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Huy ndio suarez ukizubaa anakuweka tu hana maaihara nyavuni

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Kama cjaelewa

    Jibu

    Suarez yuko vizuri sana

    Jibu

    Mwanzo mzuri sana hapo ndio Barcelona watajua umuhimu wako

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Ameanza vizuri

    Jibu

    Jambo zuri

    Jibu

    Jambo jema

    Jibu

    Suarez ni makin sana

    Jibu

    Yuko poa

    Jibu

    Suarez yupo vizuri sana

    Jibu

    Suarez mtu mmbaya

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Safiiii Sana

    Jibu

    Jambo zuri

    Jibu

    Yuko vzuri

    Jibu

    Suarez hanazidi kuonesha mahajabu yake na ndio maana Barcelona waliamua kumuuza mbali na wapinzani wao wanaijua shuuli yko

    Jibu

    Good

    Jibu

    Safi sana Suarez .

    Jibu

    Suarez yuko vizuri

    Jibu

    Safiii hiyoo

    Jibu

    deal done

    Jibu

    Safii

    Jibu

    Namkubali Sana.

    Jibu

    Mwanzo mzuri kwa Suarez

    Jibu

    Huy ndio suarez ukizubaa anakuweka tu hana maaihara nyavuni

    Jibu

Acha ujumbe