Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Juventus wameonesha nia kwa mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 32, huku mustakabali wake ukiwa shakani katika Uwanja wa Emirates baada ya kuvuliwa unahodha.

Leeds wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Juventus Mmarekani Weston McKennie lakini itagharimu takriban £20m kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23.

Mshambuliaji wa Manchester United, Edinson Cavani ndiye anayelengwa na Barcelona kwenye dirisha la usajili la Januari lakini Barca wanataka kuhakikishiwa kwamba raia huyo wa Uruguay, 34, amepona jeraha lake kabla ya kusaini mkataba.

 

Tetesi zinasema, Manchester United iko tayari kushindana na Chelsea katika kinyang’anyiro cha kumnunua mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 23, kutoka Sevilla.

Newcastle wanataka kumsajili kwa mkopo, mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial, 26, mwezi Januari, huku wakiachana na mshambuliaji wa Inter Milan na Bosnia, Edin Dzeko, 35.

Tetesi zinasema, Paris St-Germain wanajiandaa kujaribu azma ya Barcelona kumbakisha kiungo wa kati wa Uhispania Gavi, 17.

Tetesi zinasema, Newcastle wamependekezwa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Uingereza Dele Alli, 25, kwa mkopo mwezi Januari.

Tetesi zinasema, Meneja wa Tottenham Antonio Conte amezungumza na kiungo wa kati wa Inter Milan na Chile Arturo Vidal, 34, kuhusu kujiunga na klabu hiyo ya London.

Tetesi zinasema, Bayern Munich watajiunga na kinyang’anyiro cha kumnunua fowadi wa Leeds na Brazil Raphinha, 24, msimu ujao wa joto.

 

Meneja wa Roma Jose Mourinho anamtaka Tammy Abraham, 24, kusaidia kumshawishi mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, 25, kuhamia Stadio Olimpico.

Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 29, ana ndoto ya kuendelea kucheza soka tena baada ya kuondoka Inter Milan, wakala wake amesema.

Watford wanamfuatilia mlinzi wa Sampdoria na Gambia Omar Colley, 29, huku mkufunzi wa Hornets Claudio Ranieri akitaka kuimarisha safu yake ya ulinzi mnamo Januari.


ANZA MSIMU WA SIKUKUU NA BURST THE BANK

Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe