Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, inaaminika kubadili upepo kuelekea Liverpool baada ya kutohamasika na kiwango kilichooneshwa na Real Madrid katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaa dhidi ya Paris St-Germain.

Mshambuliaji wa Manchester United, mreno Cristiano Ronaldo, 37, anaweza kujikuta akicheza pamoja na hasimu wake mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 34, msimu ujao pale Paris St-Germain.

Tetesi zinasema, Real Madrid inajipanga kumsajili achezee Bernabeu mlinzi wa kushoto wa Arsenal raia wa Scotland Kieran katika dirisha la usajili ya majira ya joto.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Matumaini ya Kiungo wa West Ham na England Declan Rice, 23, ya kujiunga Chelsea yamefifishwa baada ya Thomas Tuchel kuamua kumtumia kiungo muingereza Conor Gallagher, 22, kwenye kikosi cha kwanza cha ‘Blues’ msimu ujao.

Tetesi zinasema, Newcastle wako tayari kupeleka ofa mpya kwa ajili ya mlinzi wa Sevilla, mbrazili mwenye miaka 28, Diego Carlos.

Tetesi zinasema, Arsenal na Manchester City zinafikiria kumsajili mshambuliaji muargentina wa Inter Milan Lautaro Martinez, 24 katika dirisha lijalo la usajili.

Bosi wa zamani wa Red Bull Salzburg na RB Leipzig, mmarekani Jesse Marsch ni chaguo la kwanza la Leeds United kuchukua nafasi ya kocha Marcelo Bielsa, 66, endapo klabu hiyo itaamua kuachana na kocha huyo muargentina, mwishoni mwa msimu.

Tetesi zinasema maskauti wa Newcastle United wanamfuatilia kwa karibu kinda la kimataifa la Ubelgiji Jeremy Doku, 19 ambae anachezea Rennes akitajwa kuwa na thamani ya £22m.

 

Botman

Baada ya majaribio kadhaa ya kumsajili mlinzi raia wa uholanzi, Sven Botman, 22 kuondoka Lille katika dirisha la usajili la mwezi Januari kushindwa, Newcastle United imeanza tayari mazungumzo ili kupata huduma yake katika dirisha lijalo la usajili.

Tetesi zinasema, mazungumzo yanaendelea kati ya Chelsea na wawakilishi wa mlinzi Antonio Rudiger, 28 kuhusu mkataba mpya wa mlinzi huyo wa Ujerumani ili aendelee kusalia Stamford Bridge.

AC Milan imeungana na Borussia Dortmund na Barcelona katika mbio za kumsajili mlinzi wa kulia wa Morocco Noussair Mazraoui, 24, ambaye alisema ataondoka Ajax mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa