Tetesi zinasema, Inter Miami itapambana kumsajili mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi kama nyota huyo mwenye miaka 34 ataamua kuondoka Paris St-Germain, anasema mmiliki mwenza wa klabu hiyo ya ligi kuu ya Marekani.

Mkataba wa mshambuliaji wa Poland, Robert Lewandowski pale Bayern Munich unamalizika mwaka 2023, wakati mkongwe huyo mwenye miaka 33 akitaka mkataba mpya kusalia katika klabu hiyo

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway, Erling Braut Haaland hajakubali kujiunga na Real Madrid katika dirisha lijalo la majira ya joto.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

Tetesi zinasema, Barcelona wanakaribia kumsajili kiungo wa Ivory Coast, Franck Kessie kwa uhamisho huru wakati mkataba wa nyota huyo wa AC Milan mwenye umri wa miaka 25 utakapomalizika.

Newcastle United ilishindwa kumsajili mlinzi wa Uholanzi, Sven Botman mwezi Januari, na kinda huyo mwenye miaka 22 ambaye anahusishwa pia na Tottenham, anatarajia kujiunga na AC Milan katika majira yajayo ya joto.

Andreas Christensen ameelezea suala lake ndani ya Chelsea ni gumu, huku mkataba wa mlinzi huyo wa Denmark mwenye miaka 25 ukielekea ukingoni mwisho mwa msimu.

 

Christensen

Mlinzi wa Sporting Lisbon mreno Goncalo Inacio amekubali kusaini mkataba mpya kusalia klabuni hapo. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 20 alikuwa akiwaniwa na Newcastle United katika dirisha la mwezi Januari.

Tetesi zinasema, Klabu za Real Sociedad na Atalanta zinamuwania kwa mkopo mlinzi wa kushoto mgiriki Dimitris Giannoulis kutoka Norwich City.

Tetesi zinasema, Kiungo wa zamani wa Manchester United, Roy Keane ameiambia klabu hiyo kumpa mikoba ya ukocha, kocha wa sasa wa Atletico Madrid Muargentina Diego Simeone.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa