Tetesi za Usajili

Mshambuliaj Wolves, Raul Jimenez, 28, amesema itakuwa ngumu kukataa ofa kutoka kwenye vilabu vya Hispania Real Madrid and Barcelona.

Golikipa wa Manchester United, Dean Henderson, 23, ambaye ametumikia kwa mkopo msimu 2019.20 akiwa Sheffield United, anatarajia kuendelea kutumia mwaka mwingine nje ya klabu.

Straika wa Lyon, Moussa Dembele, 23, amehusishwa kuwindwa na Manchester United lakini klabu hizi mbili hazijafanya mazungumzo.

Moussa Dembélé

Kiungo wa Chelsea, Willian, 31, amesema haina tatizo kuhamia kwenye klabu hasimu jijini London – lakini hakujata aidha ni Tottenham au Arsenal.

Winga wa Bournemouth Ryan Fraser, 26, amewaambia marafiki zake anatamani kujiunga na Tottenham kipindi hiki cha kiangazi kama watamhitaji.

Kiungo Atletico Madrid Hector Herrera, 30, ni mmoja ya wachezaji waliowindwa na West Ham katika dirisha la usajili Januari na wakashindwa kunasa saini yake, lakini bado wanajaribu kumsaini kipindi hiki cha kiangazi.

Winga wa Valencia Ferran Torres, 20, amemshauri mchezaji mwenzake Jose Luis Gaya, 24, asikubali kusajiliwa na Liverpool.

Mshambuliaji wa Barcelona, Philippe Coutinho, 27, yuko nje ya bajeti ya Leicester City, amesema kocha Brendan Rodgers, pamoja na uvumi kipindi hiki cha kiangazi.

Mchezaji mpya wa Watford Pape Gueye, 21, hataki tena kucheza Premier League pamoja na kusaini mkataba wa miaka mitano kwasababu anahofia atatolewa kwa mkopo.

Liverpool wamewasiliana na beki wa Napoli Kalidou Koulibaly, 28, kama mbadala muhimu wa Joel Matip.

Tottenham wameanza mazungumzo  ya kusaini beki wa Hellas Verona, Marash Kumbulla, 20, kama mbadala wa Jan Vertonghen.

18 Komentara

    Hawa Liverpool hawa

    Jibu

    Huwezi kataa ofa ya vilabu vikubwa kama bacelona

    Jibu

    Naona in vizuri inapotokea ofa kama hizi kwa wachezaji inakua ni fursa kwao

    Jibu

    Muda wake sasa kwenda kukipiga kwenye timu kubwa zaidi!!!

    Jibu

    Changamkia fursa hiyo Raul.

    Jibu

    Masilai kwanza

    Jibu

    anatakiwa achangamkie fursa ila kikubwa aangalie na maslai yake

    Jibu

    Fursa ya kutembea nayo

    Jibu

    Muda umefika kwenda kutafuta changamoto sehemu nyngne

    Jibu

    Raul nibora akaenda kweny timu zinazo muitaji

    Jibu

    Ni ndoto kwa kila mchezaji kuchezea timu kubwa ili kujitangaza zaid

    Jibu

    Big deal

    Jibu

    Atizame masilai Kwanza

    Jibu

    Achangamkie fulsa yake ndokinachotakiwa

    Jibu

    Hakuna mchezaji atakaye pinga kwenda timu kubwa

    Jibu

    Safi

    Jibu

    achangamkie tuu fulsa

    Jibu

    Kambi popote

    Jibu

Acha ujumbe