Kiungo wa kimataifa wa Italia Sandro Tonali (22) amefikia makubaliano na klabu yake ya sasa AC Milan, kuongeza mkataba wa kusalia klabuni mpaka mwaka 2027.

AC Milan Yamuongeza Mkataba Tonali (22)

Mkataba huo unatarajiwa kusainiwa mapema hii leo Septemba 09 na hivyo itamfanya kuwa mchezaji wa Milan kwa miaka miwili zaidi.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari za michezo Fabrizio Romano ambaye ni raia wa Italia ameposti kwenye ukurusa wake wa twitter na kuandika kuwa:

AC Milan Yamuongeza Mkataba Tonali (22)
Kiungo wa Ac Milan-Sandro

“AC Milan wamefikia makubaliano na Sandro ya kumuongeza mkataba mpaka mwaka 2027, mkataba huo utasainiwa baadae hii leo. Hakuna mazungumzo yeyote yaliyofanya na Tonali na klabu ya Uingereza kwenye dirisha la usajili majira ya joto”.

AC Milan Yamuongeza Mkataba Tonali (22)

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa