Thomas Tuchel amemtaja mchezaji wa Manchester United Paul Pogba kuwa ni moja ya kiungo bora kabisa ulimwenguni amesema hayo kuelekea mchezo wa Paris Saint- Germain dhidi Manchester United.

PSG itawaongoza United jijini Paris siku ya Jumanne kwa kuanza mbio za kuwania Champions League katika kundi H.

Kuelekea mchezo huo, Tuchel alimsifia Pogba ambaye alikuwa akihusishwa kwenda kwa mabingwa hao wa Ligue 1 kipindi cha nyuma.

“Ni moja ya viungo bora duniani,” kocha huyo wa PSG aliongea na waandishi.

“Bruno Fernandes ambaye amepiga pasi nyingi, ni moja ya timu nzuri barani Ulaya ni muhimu kuzuia Counter Attack.

“Tunataka kumiliki mpira tunataka kutumia mtindo wetu tunapaswa kucheza kwa mfumo mzuri wa pasi nyingi na kukimbiza.

Mchezaji mwenzake na Pogba wa zamani katika klabu ya Manchester United Ander Herrera pia alimwagia sifa Pogba.

Herrera ambaye aliachana na United na kwenda PSG anaamini Pogba anaweza kuwa katika kinyang’anyiro cha Ballon d’Or kama United wataanza kushinda mataji mbalimbali.

“Nadhani ana kila kitu nafaikiri nilishawahi kusema kwamba hakauna kiungo kama yeye kwa sasa,anaweza kufanya chochote ana ubora wote,” Herrera alisema.


Ondoka na Mkwanja Kwenye Tsh. 160,000,000

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu.

Soma Zaidi

29 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa