Uchambuzi: Arsenal vs Manchester City.

Mikel Arteta anairudisha Arsenal kwenye ramani, inaonesha kucheza kwa ari, kujiamini na lengo lao linaonekana kabisa, ni muda mrefu umepitia mpaka watu kuanza kuihofia Arsenal tena

Mbinu ya Mikel itakuwa ile ile kamba ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Pep pale Wembley Julai 2020, kutomruhusu City kucheza langoni kwake na kukabia chini kabisa.

Kumkabia Guardiola juu kutaifanya Arsenal kutoruhusu City wazungushe mipira na kucheza mchezo wao, kilichokuwa kinawauwa wengi ni kumruhusu Pep acheze hii iliwatesa sana EPL, Mikel hajawahi kukubali hii.

Uchambuzi: Arsenal vs Manchester City.

Lakini kukabia kwenye eneo lake Arsenal itamlipa, kwanza ataruhusu presha na City watafika, kifuatacho wakipora mpira Arsenal wataondoka kwa kaunta na wana watu wenye mbio wenye uwezo wa kutumia magepi kama Pepe na PEA

City wana shida kubwa kwenye eneo la ulinzi haswa makosa binafsi, Eric Garcia, Kyle Walker na Benjamin Mendy, makosa yao wote yamezaa mabao, ila suala la safu mbovu ya ulinzi ni suala la kimfumo zaidi, kuna kitu hakipo sawa

Fowadi za City hazishuki kukaba kama zamani wapo taratibu, hawapress eneo la juu, Kiungo cha City kiko ovyo sana Rodri hajawalipa kabisa, Fernandinho sio yule tena amechoka, hii inapelekea presha langoni mwao muda wote, mtu kama Leroy Sane naona anakosekana, Pep anajifariji na unane mkamilifu.

Arsenal mbinu yao ya asili ni lupiga pasi na kaunta, hii hawatoacha, namwona Granit Xhaka akianza huyu ni mchezaji muhimu zaidi kuliko mchezaji yoyote pale Arsenal kwa mfumo wa Arteta, kwanza ni nguzo ya ulinzi na kiungo, anajua kutimiza majukumu yake, namwona pia na Elneny pembeni yake

Thomas Partey ni mchezaji mzuri ila kuanza kwenye mechi kubwa tena eneo linaloakisi mchezo mzima wa Arsenal sioni Arteta akicheza kamari hii, nawaza Pepe dhidi ya Mendy na Auba atapewa kazi na Kyle Walker bila shaka

Nawapa nafasi kubwa Arsenal ila safu yao ya ulinzi inanitatiza sana, makosa mengi sana, hawatowazuia City wasifunge kabisa, mechi hii ina mabao mengi na nafasi nampa Arsenal.


Unapenda kuwa shujaa?

Naam, hapa ni mahali pako! Kuwa shujaa kwenye sloti hii ya Samurai Ken ujishindie mkwanja na kujipa burudani murua. 

Cheza sasa 

Samurai Ken Online Casino

26 Komentara

    Itakuwa mechi kali sana

    Jibu

    man city wasilewe sifa arseanal ya sasa si ile ya mala kwanza wajipange sana

    Jibu

    huu mechi si ngumu sana kwa arsenal kama watakua wamejipanga hipasavyo

    Jibu

    Duuh itakuwa mechi kali sio ya kitoto!!

    Jibu

    noma sana

    Jibu

    Hii mechi Arsenal akijitahidi anaweza kushinda

    Jibu

    Man city wasipoangalia watapewa sita kama wezao

    Jibu

    Mmm hiyo mechi navyo hiyo haitabiliki kwasababu Arsenal anataka ushindi Man City anataka ushindi kwaio ngoja tuone mtanange huo

    Jibu

    Itakuwa mechi muhimu kuangalia na kubashiri na endapo wakati huu Arsenal ya Arteta itashinda basi mwanafunzi atakuwa ameiva

    Jibu

    Mechi kalii sanaa ya magor

    Jibu

    Mechi kali sana

    Jibu

    Noma sana

    Jibu

    Kwa mechi kama hii ubashiri wa uhakika ni magoli tu

    Jibu

    Mechi itakuwa na upinzani mkubwa sana

    Jibu

    Itakua bonge la mechi ilo

    Jibu

    Big mechi

    Jibu

    The gunners ni moto

    Jibu

    Mechi kalii

    Jibu

    Mechi ipo 50/50 kama Arsenal watatumia mapungufu ya Mancity basi wataibuka na ushindi

    Jibu

    Kaliii kinyama

    Jibu

    Hii mechi ipo 50/50

    Jibu

    Don’t miss

    Jibu

    Bonge la mtanange

    Jibu

    Hatari hii

    Jibu

    Kivumbi na jasho

    Jibu

    Usikose hii

    Jibu

Acha ujumbe