Uchambuzi: Wolves vs Chelsea.

Frank Lampard anatarajia kukutana na Nuno Espirito Santo’s Usiku wa leo pale Chelsea itakapo kabiliana na Wolves katika mchezo wa Premier League katika dimba la Molineux.

Chelsea ilicheza mechi 17 bila kupoteza katika mashindano yote lakini mbio zao zilifikiaa tamati walipokutana Everton baada ya kukubali kipigo cha 1-0 katika dimba Goodison Park.

Taarifa ya timu ya Wolves.

Joao Moutinho amefungiwa kucheza na hatokuwa sehemu ya ziara ya Wolves kwenda Chelsea siku ya Jumanne. Kiungo huyo alitolewa baada ya kupata kadi mbili za njano katika mchezo wa Jumamosi wa 1-0 dhidi ya wapinzani wao Aston Villa.

Raul Jimenez anaendelea na hatua za mwanzo za kupona kuugua fuvu la kichwa lililovunjika mwezi uliopita na amekuwa akitumia muda na kikosi kwenye uwanja wa mazoezi wa kilabu, wakati Jonny mwenye tatizo la goti hayupo katika mchezo wa leo.

Taarifa ya timu ya Chelsea.

Christian Pulisic anarejea kwenye kikosi cha Chelsea. Winga huyo wa Marekani alikuwa nje ya dimba kutokana na shida ya nyama ya paja lakini ameanza kufanya mazoezi vizuri tangu wikendi na yuko mbioni kuanza endapo Frank Lampard ataamua kukibadilisha kikosi kilichopoteza dhidi ya Everton siku ya Jumamosi.

Wachezaji mwenzake Hakim Ziyech na Callum Hudson-Odoi wote wanahitaji muda zaidi wa kuendelea kujitizamia kutokana na majeraha yao ya nyama za paja.

Je Ulijua?

Tangu waliporejea Ligi Kuu mwaka 2018, Wolves wamepoteza michezo minne kati ya mitano waliyocheza ambayo Jimenez hakuanza.

Mshambuliaji Tammy Abraham ana mabao sita katika mechi nne za ligi dhidi ya Wolves – pamoja na hat-trick katika ushindi wa 5-2 huko Molineux msimu uliopita.

Baada ya kutikisa nyavu mara saba katika michezo saba ya awali, mshambuliaji wa Chelsea Timo Werner sasa hajafanikiwa kufungaa katika michezo saba sasa.


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

15 Komentara

    mambo ni moto na meridianbet

    Jibu

    Habari hipo vizuri

    Jibu

    Mechi sio ya kukosa kabisa chelsea watatoka kweli

    Jibu

    Habari nzuli

    Jibu

    Mechi sare hii

    Jibu

    Habari ilo poa

    Jibu

    Asant kwa uchambuzi

    Jibu

    Asnt kwa taarif meridianbet

    Jibu

    Habari safi

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Guud

    Jibu

    Lampard alipotea sana hii mechi

    Jibu

    Gud

    Jibu

    Good news

    Jibu

    ulikuwa poa sna

    Jibu

Acha ujumbe