United Yavunja "Unbeaten" ya Arteta

Klabu ya Manchester United ambayo ipo chini ya kocha mkuu Erick Ten Hag imevunja rekodi ya Arsenal ya kuwa timu ambayo haijapoteza mchezo wowote wala kutoa sare msimu huu toka ligi kuu ya Uingereza ilipoanza.

United Yavunja "Unbeaten" ya Arsenal

United waliwaleta The Gunners nyumbani kwao pale Old Traford majira ya 18:30 ambapo katika kipindi cha kwanza vijana wa Ten Hag walipata bao la kuongoza kupitia Antony, kabla ya bao la Martinelli lililofungwa na  The Gunners kukataliwa na VAR kipindi hicho cha kwanza.

Arsenal mpaka kufikia mechi ya jana ya sita ilikuwa ni timu pekee ambayo imeshinda michezo yake mitano huku akiwa pale kileleni katika msimamo. Hadi kufika dakika 90 za mpira kumalizika ile Unbeaten ya Arsenal ilivunjwa rasmi na mashetani wekundu huku akipoteza kwa mabao 3-1

United Yavunja "Unbeaten" ya Arsenal

Mpaka sasa united wameshinda mechi nne mfululizo kwenye ligi kuu ya Uingereza huku sajili zao walizofanya zikionekana kuzaa matunda, Ameshinda dhidi ya Liverpool, Leicester City, Southampton na hapo jana aliposhinda dhidi ya Arsenal.

Lakini pamoja na The Gunners kupoteza mchezo wao wa kwanza bado wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wakiwa na alama 15 huku akimpita alama moja tu Manchester City ambaye yupo nafasi ya pili, huku United akipanda hadi nafasi ya tano akiwa na alama 12.

Acha ujumbe