Utani Wa Matthaus Kuhusu Messi na Argentina.

Ujerumani watampa Lionel Messi pasipoti ya kusafiria kama atajihisi kutokukubalika na taifa lake, aliongea katika hali ya utani Lothar Matthaus, ambaye angependa kuona Messi akicheza katika ligi ya Bundesliga.

Messi ameshinda mataji 34 akiwa na Barca, lakini ameshindwa kuyafikia mafanikio hayo katika timu ya taifa kwa kupoteza fainali nne kubwa akiwa ana timu ya Taifa bado anapambana kuleta kombe kwa timu ya taifa iliyo shinda tangu mwaka 1993.

Ukweli ni kwamba muda mwingi Messi ametumia maisha yake kuwa Spania, na mara nyingi amekuwa akikosolewa na Argentina kwa kushindwa kuipatia mataji ya kimataifa kama vile Kombe la dunia na Coppa America.

Messi amekuwa akifananishwa na mtaifa mwenzake Diego Maradona, ambaye hakupata mafanikio mengi katika ngazi ya klabu lakini alipelekea Argentina kushinda kombe la Dunia mwaka 1986.

Matthaus ameongelea kuwa jinsi Messi anavyo chukuliwa na  taifa lake ametoa maoni kuwa Ujerumani ipo tayari kumpa Uraia.

“Siwezi kuamini hii, kama humtaki Messi anaweza kuja Ujerumani muda wowote, tunasubiri jambo hilo litokee tutampa Pasipoti. Nashindwa kuwaelewa ,” aliiambia Nacion Matthaus ambaye alishinda kombe la Dunia na Ballon d’Or mwaka 1990.

“Mazungumzo ni yale yale kati ya Messi au Maradona yupi ni bora . Argentina wana bahati kupata wachezaji hawa wawili wakubwa, na wanabishana yupi ni bora kati yao? Tafadhali.“Wanawachezaji wawili pekee wakubwa katika historia ya mpira nchini mwao.”

Imekuwa ikiripotiwa kuna kipengele kitacho mruhusu Messi kuondoka Barca kwa uhamisho huru akimaliza msimu.

Messi mwenye umri wa miaka 33 anatarajia kuongeza mkataba hapo Camp Nou, lakini Matthaus amgependa kumuona mtaalamu huyo akisakata kabumbu katika ligi ya Bundesliga

“Kwakweli tungemchukua, tungefurahia kama tungepata nafasi ya kuwa na Leo katika ligi ya Bundesliga,” alisema Matthaus.

“Lakini nakubaliana nao: Nina furaha kuwa na mtu kama Messi kwenye kandanda.Ni mchezaji mkubwa na ni mtu mzuri sana.

“Namfahamu Messi binafsi na ananifurahisha na mtindo wake wa uchezaji.”

 

39 Komentara

    mess bila Barcelona hawez kufanya lolote

    Jibu

    Kujikwaa ukaanguka hakumaanishi safari ndo imeishia apo ata Messi atajiangalia wapi alikosea ili ajisahahihishe afikie malengo

    Jibu

    Matthau’s yupo sawa kwa kuwa Messi ni mchezaji mzuri sana kama muandishi anavyosema kuwa anamataji 34 aliyopata kwenye timu yake ya klabu ya barcellona,Messi alitaka kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina Ila raia wa Argentina hawakutaka kumuona Messi kuacha kucheza katika timu yao ya taifa licha ya kufanya vibaya katika timu yake ya taifa mashabiki bado wanampenda sana,MATTHAUS alitamani Messi anyone Ujerumani hahaha kitu ambacho hakiwezekani

    Jibu

    Messi atabaki kuwa muagentina tu

    Jibu

    Messi Barcelona ndo nyumba kwao! Huyo atamalizia soka lake hapo caturunya.#meridianbettz

    Jibu

    Mess ni lazma aendelee kubaki Barcelona agentina ni nyumani

    Jibu

    Messi bila Barcelona awezi kufanya lolote Barcelona ndio mama kwampambanaji huyo

    Jibu

    Mess ni mzuri sema anatakiwa aende kwenye ligi nyingine akutane na challenge
    Mpya aonyeshe ubora wake

    Jibu

    Messi ni mchezaji nzuri kwenye klabu sio timu ya Taifa.

    Jibu

    Duuh hatari sana kumbe barcelona ndio imemuinua messi basi kumbe arudi barcelona ili akaendelee kufanya maajabu

    Jibu

    Messi inabidi atoke Barca aende klabu nyengine ili apate changamoto nyengine

    Jibu

    Messi popote anafit tu

    Jibu

    Yuko sahihi matthaus kwake anatamani messi aende ujeruman lakini pia akumbuke kuwa messi hawezi kwenda mechi nyingine zaid ya Barcelona ingawa alishawishiwa na kikosi hicho kusaini mkataba wa kudumu na kuukataa inavyoonekana messi anataka acheze hapo Barcelona mpaka atakapo staafa ingawa utani unaleta chachu ya Mabadiliko

    Jibu

    Barelona wanamtegemea sana messi

    Jibu

    Messi na Barcelona ndo panamfaa

    Jibu

    Messi na Barcelona, Barcelona na Messi

    Jibu

    Vituko hivi

    Jibu

    Anachangamoto moja tu hispania bhas mnatarajia aisaidie team ya taifa kubeba ndoo?

    Jibu

    Messi mchezaji wakimatifa …akii tu n Barcelona

    Jibu

    Japo tunaweza kusema utani lakini Matthau’s alichokiongea yuko sahihi sana kwa staa huyo maana kuna kipindi kulikuwa kunaskendo nyingi sana kumuhusu messie na baba yake kutolipa kod na baadhi ya skendo kibao ambazo linamfanya star huyu kushushwa hadhi yake kwa kitendo cha kuongea hicho alimaanisha kabisa
    Maana star Kama huyu alipaswa kupewa heshima kubwa sana katika taifa lake Kama mastaa wengine Kama Zidane ambaye alitengenezewa had Sanam ,mwingine Neymar ,CR 7 na wengine wengi tunaona mataifa yao wakipewa heshima kubwa sana hivyo natambua Kama kwel messie angepata uraia wa ujeruman na kwa uwezo wake basi ata sanamu ya Messi ingetengenezwa huko ujeruman
    Kwa upande wangu naamin Matthau’s alikuwa anaongelea utani kwa kumaanisha Jambo la kwel
    Hv nice update 👍
    # meridianbet Tanzania

    Jibu

    Messi na barcelon ndio panamfaa#meridianbettz

    Jibu

    Messi inabidi aende klabu nyengine abadili upepo kidogo

    Jibu

    Kila mpenzi wa mpira atakwambia Messi ana vitu adimu kwa wachezaji wa siku hizi ni bahati mbaya hajapata mafanikio katika timu yake ya Taifa#meridianbettz

    Jibu

    Messi na Barcelona damdam

    Jibu

    Kinachomshinda Messi kupeleka ubigwa kwao Wenzake hawana bidii sana#Meridianbettz

    Jibu

    Maoni:mwenyewe inaonyesha mapenzi yake yapo Argentina.

    Jibu

    Anaweza tuu kufanya hvyo maana inaonesha timu yake ya taifa argentina kama diego costa tuu kwenda spain

    Jibu

    Messi popote pale anapawasha kwani mwanajeshi hachagui uwanja wa vita messi jembe Sana

    Jibu

    Ukiangalia Sana Kama kweli ni utani lakini ni kweli kabisa

    Jibu

    Popote kambi kwani Messi ni fundi ambae haogopi chochote

    Jibu

    Mess na Barcelona damdam

    Jibu

    Mess ni wa Barcelona tuu hakuna cha zaidi

    Jibu

    Star kama messi alipaswa kupewa heshima kubwa sana katika taifa lake kama mastaa wengine wakina neymar,cr7,zidane na wengine wengi tunavyo on a mataifa yai wakiwapa heshima..!matthau’s alikua hanaongea utani wa kumaanisha na ukweli

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Utani unaweza kuwa kweli

    Jibu

    Mess aitaji changamoto me naon akitok Barca analud kwao Argentina

    Jibu

    Abaki hapo hapo ana miaka mingi ya kuzeeka

    Jibu

    Ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Abadili upepo kila siku Barcelona na Argentina timu nyingine zinamuitaji ingawa itakuwa ni vigumu kwa Barcelona kumuondoa mess

    Jibu

Acha ujumbe