Vilabu vya Premier League vipo hatarini kukosa udhamini kutoka kwa makupuni ya Ubashiri/beti baada ya serikali ya Uingereza kutaka kufungia ushawishi wa kucheza kamari kwenye ulimwengu wa soka kwa kuonekana kwenye jezi za timu zao.

Takribani vilabu 20 vya EPL vinadhaminiwa na makupuni ya ubashiri ambao katika sekta hiyo wanazalisha zaidi ya euro bilioni 16.

Kwa hiyo kufungiwa kwa makampuni hayo kutasababisha hasara ya takriban euro 44m kwa kila klabu.

Watu milioni tatu wanasemekana kuathiriwa vibaya na ulimwengu wa kamari, serikali ya Uingereza inafikiria kupiga marufuku kampuni za kamari kuonekana kwenye jezi za timu na hii inaweza kutokea ifikapo 2023 au 2024.

Ingawa marufuku ya kuonekana kwa makampuni ya beti kwenye jezi bado haijaanza, itakuwa badiliko kubwa zaidi kwa mikataba ya udhamini tangu utangazaji wa tumbaku ulipigwa marufuku mwaka wa 2003.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa