Waacheni Yanga Watambe, Walikua Vibaya Misimu Minne

Ukisoma history utagundua mwaka 1929 kulitokea anguko kubwa sana la uchumi duniani (GREAT ECONOMIC DEPRESSION) hii ilihusisha mataifa yenye nguvu kipindi hiko kiuchumi kuanguka kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo first world war ile ya mwaka 1914 hadi 1918.

YANGA

Sasa Nchi kama British,Germany,Russia na nyingine kubwa zilianguka kiuchumi hivyo kupelekea Great economic depression, sasa kwenye kurudi kwenye ubora wa mwanzo ilitakiwa wapitie hatua kama recovery badae boom.

Young Africa ilipitia economic depression kwa miaka isiopungua mi nne kabla ya kuijenga hii yanga inayofanya vizuri sasa hivi kwenye ligi.

Kwa miaka yote mi nne yanga walikosa ubingwa hii ilitokana na anguko la uchumi huku yanga ikikosa nguvu ya kupambana na mpinzani wake mkubwa simba kwenye kusajili wachezaji wenye ubora na quality ya kuchezea yanga.

Simba alitawala ligi ya Tanzania kwa miaka isiopungua mi nne kwasababu alikosa ushindani wa kweli kutoka kwenye klabu nyingine zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara na hii ni kwa sababu ya anguko kubwa la uchumi, kutowalipa mishahara wachezaji na kukosa kuendesha timu kiujumla ikiwemo kusajili wachezaji bora na wenye tija.

Kwanini nasema Dar es Salaam Young Africa  ilipitia great economic depression na leo wapo kwenye recovery stage? recovery ni stage ya pili kutoka kwenye depression na boom ni kilele cha mafanikio sasa yanga wapo kwenye recovery stage.

Baada ya anguko kubwa kwa muda wote yanga walipata mwekezaji GSM ambae ameifanya Young Africa kusajili wachezaji wenye ubora wa kuchezea yanga na kuleta ushindani kwa timu zingine, leo yanga anaongoza ligi na anacheza vizuri sio kwa bahati Mbaya Ila ni kwa matokeo ya kusajili wachezaji bora na wenye uwezo wa kuipambania nembo ya yanga.

Kilele cha Young Africa (boom) ni kuchukua ubingwa wa ligi kuu waliokosa kwa muda mrefu na hii ndio itakuwa hatua ya mwisho kwa Young Africa wametoka kwenye depression sasa wapo kwenye recovery stage wanahitaji kuchukua ubingwa wa ligi kuu ili wawe wamefanikiwa kujitoa kutoka kwenye anguko kubwa.

Wanacheza vizuri na wanaongoza ligi ila bado wapo kwenye recovery stage wakichukua ubingwa basi watakuwa kwenye Boom stage.

Imeandikwa na Ashraf Junior.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

Acha ujumbe