Radja Nainggolan, Robert Gagliardini na Ionut Radu wote wamekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona baada kufanyiwa vipimo, klabu ya Inter imetangaza.

The Nerazzurri wametoa taarifa siku ya Ijumaa, siku nane kabla ya kuelekea mchezo wa debi ambapo watakabiliana na mahasimu wao Milan, wamesema wachezaji hao watatu walionesha dalili za kuwa na maambukizi ya COVID-19.

Vipimo kwa wachezaji hao vilifanyika klabuni katika makao makuu ya viwanja vya mazoezi vya Appiano Gentile.

“FC Internazionale Milano inatangaza kwamba Radja Nainggolan na Robert Gagliardini wamekutwa na maambukizi ya COVID-19 baada ya kufanyiwa vipimo Appiano Gentile siku za hivi karibuni,” Inter walisema.

“Ionut Radu pia amekutwa na maambukizi asubuhi ya leo (Ijumaa) baada ya kufanya zoezi la upimaji jana vipimo zaidi vitaendelea siku ya kesho.

Kiungo Gagliardini alianza katika michezo miwili iliyopita ya Serie A kwa Inter na alifanikiwa kufunga goli moja na kutoa asisti katika ushindi wa 5-2 wa Inter Milan dhidi ya Benevento mwezi Septemba 30.

Nainggolan alirejea San Siro msimu huu baada ya kutumia msimu uliyopita na Cagliari kwa mkopo, ingawa alicheza dakika 15 pekee akitokea benchi kwenye mchezo dhidi ya Fiorentina.

Mlinda mlango wa ziada Radu hajawahi kuanza kwenye michezo ya Serie A na alicheza mchezo pekee wa ligi katika timu ya Inter alitokea sub mwaka 2016.


Weka Pesa kwa Airtel Money!

Sasa unaweza kuweka pesa moja kwa moja kwenye akunti yako ya Meridianbet kwa kutumia mtandao wa Airtel. Usipate wasi wasi, tunaifanya kazi kuwa rahisi zaidi!

Soma Zaidi

36 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa