Klabu ya West Ham wanaendelea kuboresha kikosi chao wakati wa dirisha hili linaloendela la usajili sasa wameandaa kiasi cha pauni milioni 30 kumnunua Nayef Aguerd kutoka Rennes.

West Ham Mbioni Kukamilisha Usajili wa Nayef

Mchezaji huyo wa Morocco amecheza mechi 66 kwa Rennes baada ya kujiunga na klabu hiyo mwaka 2020 akitokea Dijon akiwa amefanikiwa kufunga mabao 5 na kusaidia mengine matatu.

Nayef aliagwa na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii ambapo mchezaji huyo wa miaka 26 aliandika “Ni maamuzi magumu kuondoka Rennes ambako nilifurahia wakati wa kipekee huko”.

Anatarajia kufanyiwa vipimo vya afya siku ya Jumatatu na kama dili ya Nayef ikikamilika basi utakuwa usajili wa nne wa gharama kwa West Ham baada ya Sebastien Haller, Felipe Anderson na Kourt Zouma kusajiliwa kwa pesa ndefu.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa