Mchezaji wa Arsenal anayechezea kwa mkopo klabu ya Ufaransa Marseille William Saliba ameitaraarifu klabu ya Marseille nia yake ya kutaka kubaki kwenye klabu hiyo licha ya kuhakikishiwa nafasi ya namba kwenye klabu hiyo ya London msimu ujao.

William Saliba alijiunga na klabu ya Marseille kutoka Arsenal kwa mkopo wa muda mrefu na amefanaikiwa kuichezea klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa Ligue 1 michezo 51 kwenye mashindano yote msimu huu mpaka sasa.

William Saliba
William Saliba

Saliba amekuwa moja ya mchezaji muhimu kwenye klabu ya Marseille na amekuwa chachu ya kuifanya timu hiyo kuweza kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa ulaya, pia amekuwa mchango mkubwa kuifikisha timu hiyo nusu fainali ya  Europa Conference League.

Ijapokuwa klabu ya Arsenal imevutiwa na kiwango alichokiomyesha akiwa kwenye klabu ya Marseille lakini William Saliba hana mpango wa kurudi kwenda kufanya kazi na Arteta na tayari ameshaweka wazi hilo kwa kuzungumza nia yake ya kutaka kubaki nchini Ufaransa.

Kulingana na  RMC Sport, Mlinzi huyo wa kati ameumbia uongozi wa klabu hiyo kuwa anahitaji kubaki, pia kocha Jorge Sampaoli ameonesha nia ya kutaka kumbakisha William Saliba kwenye klabu hiyo na hichi ndicho kipaumbele chake kwa sasa.

Mapema mwezi huu wakati alipopata nafasi ya kuhojiwa kuhusu kurejea Marsielle alijibu, “hitaji langu ni kumaliza msimu vizuri, kuondoka vizuri endapo sitarajea tena.

“Itakuwa vizuri mimi kurudi tena hapa haijarishi itakuwaje, sio kwamba sitarejea tena Marseille, ni klabu yangu.”


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa