UONGOZI wa Yanga umetuma ujumbe mbaya kwa watani zao wa jadi Simba baada ya kuweka wazi kwamba msimu ujao wanahitaji kubeba mataji yote matatu ambayo wameyatwaa.

Ikumbukwe kwamba Yanga imetwaa taji la Ngao ya Jamii,Kombe la Shirikisho na Kombe la ligi ambapo msimu wa 2020/21 yote yalikuwa mikononi mwa Simba.

Akizungumza na Championi Jumamosi,Kaimu Mtendaji wa Yanga, Senzo Mbatha alisema kuwa wanatambua kwamba msimu ujao utakuwa mgumu lakini wanahitaji kutwaa mataji yote matatu.

“Msimu ujao tena kwa wakati mwingine tunahitaji kuweza kuyatwaa mataji yote matatu na tunatambua kwamba utakuwa na ushindani mkubwa msimu ila tunahitaji kutwaa mataji yote matatu kwani uhitaji bado ni mkubwa.

“Mashabiki wanapenda kuona mafanikio ambayo yanapimwa kutokana na kile tunachokifanya hasa uwanjani,hakuna ambaye hapendi kuona tunafurahi hivyo ni muda wetu kuwa kwenye mwendelezo wa furaha,” alisema Mbatha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa