MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally amesema kuwa watachokwenda kukifanya kesho mbele ya Kagera Sugar ni kupiga mpira mkubwa na kusaka matokeo ya ushindi mnono.

Ahmed Ally
Ahmed Ally
Ahmed Ally aliongeza kuwa wanafahamu ubora wa Kagera Sugar kwani ni kati ya timu ambazo ziliwafunga msimu uliopita, hivyo hawataki tena kuwapa huzuni mashabiki wao ambao walianza msimu kwa furaha na amani.

Ahmed alisema kupata kwao alama tatu na mabao 3-0 mbele ya Geita Gold siku chache zilizopita, inawapa sababu ya kuendelea kutoa burudani kama hiyo kwa mashabiki, kwani Simba ni timu ambayo inatakiwa kushinda mara zote na siyo kufungwa.

Ahmed Ally
Ahmed Ally

“Kagera Sugar tunawafahamu kuwa ni timu bora na ina wachezaji wazuri kwenye kila eneo. Lakini tunakwenda kuwapigia mpira mkubwa sana kwa sababu hatutaki kurudia tena makosa.

Mashabiki wa Yanga na wapenda mpira mzuri na hata kama unatoka upande wa pili unaruhusiwa kuja na kuona burudani hii ya mpira mkubwa Tanzania,” alisema.


Kwa Taarifa za Burudani na Uchambuzi tembelea kwenye Youtube ya Meridianbet au Gusa Video Hii.
https://www.youtube.com/watch?v=MENhy-HIEF8 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa