Viongozi wa Simba wameweka wazi kuwa licha ya kuwa kuna wachezaji watakosekana kwenye mechi yao dhidi ya Big Stars kesho akiwemo Clatous Chama ambaye amefungiwa na TFF kucheza mechi tatu za ligi, wao wamesema kuwa ilipofikia Simba hawezi kutegemea mchezaji mmoja.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally ambaye amesema kuwa licha ya kuwa kuna wachezaji muhimu watakosekana kwenye mechi yao na Singida Big Stars, watashinda kwa kuwa Simba haitegemei mchezaji mmoja.

simba, Ahmed Ally: Simba Haitegemei Mchezaji Mmoja Tu, Meridianbet

Ahmed alisema: “Kukosekana kwa wachezaji muhimu ambao wapo kwenye majeraha na masuala mengine tunapokea kama timu na ni suala la kawaida.

“Simba haiwezi kutetereka kwa sababu ya Fulani hayupo, ndiyo tutakosa mchango wake kwenye timu ambao ungesaidia kurahisisha kupata ushindi. Lakini haina maana kuwa tutafungwa, hii timu ina kikosi kipana.”

Simba watamkosa Chama leo kwenye mchezo wao na Big Stars baada ya kufungiwa mechi tatu na faini ya shilingi laki tano na TFF sambamba na kiungo wa Yanga Stephen Azizi Ki kwa kushindwa kusalimiana na wenzao kwenye dabi ya Kariakoo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa