Beki wa Switzerland Manuel Akanji amesisitiza kuwa kikosi chake kiko tayari kuwapa ugumu wenyeji Canada katika mchezo wa mwisho wa Kundi B wa mashindano ya Dunia, akionya kuwa hakuna mechi rahisi katika hatua hiyo ya mashindano.
Canada wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na morali kubwa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Qatar, lakini Akanji amesema Switzerland haitakuwa timu ya kupuuzwa. “Tunajua wanataka kushinda, lakini sisi pia tunataka kushinda hapa. Hatutawarahisishia,” alisema.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Beki huyo aliongeza kuwa Switzerland italazimika kucheza kwa umakini mkubwa ili kupata matokeo. “Tutaweka juhudi zetu zote kesho. Nikifikiri tukionyesha kiwango chetu bora, tunaweza kushinda,” alisema, akisisitiza kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwa pande zote mbili.
Switzerland inahitaji angalau sare ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele, wakati Canada wakihitaji ushindi au sare ili kumaliza kileleni mwa Kundi B na kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza.
Akanji aliongeza kuwa nguvu ya timu yao ni kushirikiana kwa pamoja. “Hatuna wachezaji watatu bora duniani kama mataifa mengine, lakini tunafanya kazi kama timu. Tunajifunza kutoka makosa yetu na kujaribu kuwa na uthabiti,” alisema, akisisitiza matumaini ya kufanikisha hatua ya 16 bora.


