Alexander Isak anatarajiwa kuthibitishwa kama ni mchezaji wa Newcastle siku ya Ijumaa ya Agosti 26.

Mshambuliaji huyo wa Uswizi (22), aliwasili kaskazini mashariki siku ya Alhamisi na kukamilisha uchunguzi wa afya baada ya Real Sociedad kukubali dau la paundi milioni 60 kutoka kwa klabu hiyo ya Ligi kuu ya Uingereza.

alexander isak, Alexander Isak Kutambulishwa leo Newcastle., Meridianbet

Isak, ambaye amefunga mabao 44 katika mechi 132 akiwa na La Real, amekuwa kwenye rada za vilabu vikubwa vya Ulaya kwa muda sasa, huku Arsenal wakihusishwa hapo awali.

Isak alipata kutambulika kimataifa kwa uchezaji wake akiwa na Sweden kwenye Euro 2020 mwaka jana, na amefunga mabao tisa katika mechi 37 alizocheza.

alexander isak, Alexander Isak Kutambulishwa leo Newcastle., Meridianbet

Mshambuliaji huyo alihama kutoka AIK ya nyumbani kwao hadi Borussia Dortmund akiwa na umri wa miaka 17 mwaka 2017, lakini alishindwa kufanya vyema kabla ya kusajiliwa kwa mkopo katika klabu ya Uholanzi Willem II.

alexander isak, Alexander Isak Kutambulishwa leo Newcastle., Meridianbet

Isak baadaye alijiunga na Real Sociedad na ameisaidia timu hiyo kujiimarisha kama mshindani wa mara kwa mara wa soka la Ulaya, huku pia wakishinda Copa del Rey 2020, ambapo Isak alikuwa mfungaji bora wa shindano hilo akiwa na mabao saba.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa